Maharusi
Denis na bi Joviety wakiwa ibadani muda mfupi kabla ya kufunggishwa
ndoa kanisani hapo.Picha na Vero Igantus Blog
Maharusi
hawa bwana Charles na bi Sabilina waliweza kufunga ndoa katika
mkesha huo wa sikukuu ya christma katika kanisa la Katoliki Sent Treza
Jimbo la Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
|
Na,Mahmoud Ahmad.Arusha.
Wito umetolewa kwa wanaume kuwa makini na kuwasindikiza wake zao kiliniki wakati wakiwa wajawazito kwani yapo mambo muhimu watakayojifunza wakiwa pamoja yatakayomsaidia mama na mtoto kuwa salama hadi wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na father Festus Makwame wa kanisa katoliki Sent Treza jimbo la Arusha alipokuwa kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya krismas na kusema kuwa wanaume wengi hawana tabia ya kuwa na wake zao pindi wanapokuwa wajawazito jambo ambalo ni kosa kubwa
“Wanaume wasindikizeni wake zenu kiliniki huoni kwamba anashirikiana na Mungu katika uumbaji tena anakujengea heshima yawewe kuitwa baba Fulani?nenda nae yapo mambo mengi mtakayoelekezwa hata namna ya vyakula anavyotakiwa kula akisahau kwa vile ulikuwepo utamkumbusha?hebu igeni mfano wa Joseph na Maria hadi Yesu Kristo anazaliwa walikuwa pamoja.”alisisitiza
Amewataka waumini waliohudhuria ibada hiyo ya mkesha wa christmas waamue kubadilika waruhusu Kristo azaliwe mioyoni mwao ili mambo yao yawe mapya ,huku akisisitiza msamaha wa kweli pale mmoja anapomkosea mwingine kwani ni jambo ambalo Mungu analifurahia
“Wacha tuwe wakweli hakuna jambo gumu kama kumsamehe mtu aliyekukosea tena kwa makusudi,lakini kwa vile Mungu ameagiza tusameheane ni lazima tufanye hivyo na ukweli utabakia kuwa hivi Msamaha wa kweli ni ule ambao unautoa huku Unauma umekosewa lakini unasamehe kwa faida yako mwenyewe pia.”Alisisitiza father Festus.
Aidha amesema kuwa katika ibada hiyo ya mkesha wa krismas amewataka waumini kuachana mila na desturi potofu ambazo hazimpendezi Mungu kwani ni uvuli wa mauti.
“Wacheni michanganyo michanganyo kwani haimpendezi Mungu jamani kama umeamua kuwa kwa Mungu ,basi mfuate ili upate uzima wa milele ,na kama mwenzetu umeamua kumfuata shetani basi mfuate uangamie kwaani mambo haya ya michanganyiko michanganyiko mkiiendekeza huwa inaleta balaa na mikosi katika familia zenu”alisema father Festus.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni