KIMBUNGA CHAKATISHA HOTUBA YA ZUMA BAADA YA HEMA KUANGUKA

 
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelazimika kukimbia kuokoa maisha yake baada ya hema alilokuwa akitumia kutoa hotuba kuanguka.

Kimbunga hicho kilichoambatana na mvua kililichana na kuliangusha hema hilo ambalo rais Zuma alikuwa akitoa hotuba katika Siku ya Upatanishi.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya jamii inaonyesha watu wakihaha kusalimisha maisha yao wakati hema hilo likipeperushwa juu na upepo, na rais Zuma kukimbizwa sehemu salama.

Hakuna taarifa za awali zilizopatikana iwapo kulikuwapo na watu waliojeruhiwa wakati wa kimbunga hicho huko Gopane nchini Afrika Kusini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni