- Mwasilisha
mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na
wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha
hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.
- Sehemu
ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na
wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.

- Meneja
Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace
Kisetu (kushoto) akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.
- Mwasilisha mada akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) inakutanisha watendaji mbalimbali na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuangalia changamoto za kijinsia zilizopo kwenye sera za sekta tajwa.
Watendaji hao na wataalamu wanaoungana na wengine kutoka Halmashauri zote za jiji la Dar es Salaam pamoja na wanajamii kuangalia changamoto za kijinsia lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma ndani ya sekta hizo.
Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wataalamu hao Meneja Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu alisema lengo kubwa la majadiliano hayo ni kushauriana namna bora ya utekelezaji wa sera katika sekta hizo zinazotegemewa zaidi na jamii.
Wataalamu hao watatoka na kikosi kazi cha wataalamu ambacho pamoja na mambo mengine kitaweka mikakati ya pamoja ili kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa sera kwa wadau anuai.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni