Wahadhiri wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) wakiwasili katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). 
Makamu
 wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Prof Faustine Bee akimuongoza
 Mkuu wa Chuo  hicho Pius Msekwa wakati akiwasili katika uwanja wa Chuo 
hicho kwa ajili ya Mahafali ya Pili .
Mwenyekiti
 wa Baraza la Chuko Kikuu cha Ushirika Moshi,Prof Gerald Monela 
akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika 
katika uwanja wa michezo wa chuo .
"Kwa
 Mamlaka niliyokabidhiwa ,natangaza mkusanyiko huu kuwa ni Mahafali ya 
Pili ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi" haya ni maneno aliyokuwa akiyatoa
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Pius Msekwa. 
Makamu
 wa Mkuu wa Chuo  kikuu cha Ushirika Moshi ,Prof Faustine Bee (Kulia0 
akisoma ujumbe kutoka kwa Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha 
Ushirika Moshi.Basil Liheta (kushoto).
Mkuu
 wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Spika Mstaafu ,Pius Msekwa 
akiwapongeza watumishi wa Chuo hicho waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu 
katika vyuo mbalimbali. 
Makamu
 wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof Faustine Bee 
akimkaribisha Mkuu wa Chuo hicho,Pius Msekwa kuunda mkusanyiko kuwa 
Mahafali ya Pili ya Chuo hicho kwa minajili ya kutunukisha vyeti 
mbalimbali . 
Baadhi
 ya Wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi wakiwa katika 
Mahafali ya Pili ya chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa chuo 
hicho. 
Baadhi
 ya Wahitimu wa Shahada,Stashahada na Astashahada wakihudhurishwa wakati
 wa mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). 
Wahitimu
 ya Shahada ya kwanza ya Sheria wakifurahia jambo na Wahadhiri wao 
(kushoto) Shadrack Madila na George Sizya  katika mahafali hayo. 











Hakuna maoni:
Chapisha Maoni