Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo za Afrika. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo za Afrika. Onyesha machapisho yote

Ellen Johnson Sirleaf kukabidhiwa tuzo ya Mo Ibrahim

Tuzo ya uongozi bora ya Mo Ibrahim kwa viongozi wastaafu barani Afrika kwa mwaka huu inakwenda kwa rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnston Sirleaf. Hafla ya kumtunuku inafanyika mjini Kigali Rwanda.
Mo Ibrahim ambaye amekuwa akitoa tuzo ya uongozi bora kwa viongozi wastaafu barani Afrika amesema bara hilo linakabiliwa na uongozi usiozingatia maslahi ya raia walio wengi huku sekta binafsi ikitelekezwa.
Tuzo ya uongozi bora ya barai Afrika ya Mo Ibrahim ya mwaka huu inatazamiwa badaye jioni ya leo kupewa Rais wa zamani wa Liberia Johnson Sirleaf. Hafla itaongozwa na  Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika, huku akiwepo Rais wa Ivory Coast Alassane Ouatarra ambaye ni mwenyekiti jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika yuko mjini Kigali kuhudhuria khafla hiyo.
Festus Mogae (picture-alliance/ dpa) Rais wa Botswana Festus Mogae, aliwahi kushinda tuzo ya Mo Ibrahim
Mo Ibrahim amesema kwamba kukosekana kwa utashi wa kisiasa na ukosefu wa uongozi kwa maslahi ya raia walio wengi ni jambo ambalo limezuia bara hilo kupiga hatua ya maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
"Hilo ni suala ambalo kamwe huwa halijadili wazi,nani anatoa huduma?nani anatoa elimu,nani anatoa ushirikiano kwenye kila sekta?Ni mwananchi ambaye serikali ambayo wakati haimzingatii kwenye sera zake,hao ni mashujaa ambao daima hatuwazungumzii, na wakati umefika tuwazungumzie", amesema Mo.
Tuzo ya Mo Ibrahim ya dola milioni tano za Marekani hupewa viongozi waliojitahidi kuweka mazingira ya uongozi bora ya utawala wakati wakiwa madarakani.
Hata hivyo tangu ilipoanza kutolewa tuzo hii mwaka 2007  alipotunukiwa  Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano wadadisi wanahisi haijaleta mabadiliko makuwa kwenye sekta za utawala bora barani Afrika, lakini Denittah Ghat ambaye kwenye bunge la Kenya anasema wakati kama huu ni nafasi nyingine ya viongozi kujitathmini ikiwa wanafanya vema katika uongozi.
Kenia Mo Ibrahim verkündet den Gewinner des Preises 2015 (picture-alliance/AP Photo/B. Curtis) Mo Ibrahim mwanzilishi na mwenyekiti wa wakfu wa Mo Ibrahim
"Hii ni nafasi nzuri nay a kipee na ninafurahi kwamba sasa tunakutana hapa kujadili hata nafasi ya mwanamke ktk uongozi barani Afrika tunafahamu kumekuwepo na udhaifu kwa baadhi ya serikali kuwapa nafasi wanawake ambao kimsingi ni wachangiaji wa zuri kwenye maendeleo lakini nadhani kukutana hapa nadhani ni fursa nyingine kulitathmini hili".
Kutolewa kwa tuzo hiyo kumefungua kikao cha siku tatu cha viongozi wa serikali na wale wa kiraia zaidi ya elfu moja kutoka barai Afrika wakijadiliana ushirikiano unaopaswa kuwepo baina ya serikali na sekta binafsi. Rais mstaafu  Sirleaf anapewa tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake katika  kurejesha amani na usalama nchini Liberia na pia hatua yake ya kutojiingiza kwenye siasa za ushawishi kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopita nchini Liberia ambapo mwanasoka wa zamani George Weah  alimshinda aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Joseph Boakai.
Ni tuzo ambayo hutolewa kwa viongozi walioondoka madarakani kwa mujibu wa katiba  au kwa utashi wao. Hata hivyo mwaka  2009,2010,2012,2013.2015 na 2016 jopo la majaji wa wakfu wa Mo Ibrahim lilishindwa kumpata kiongozi  aliyefaa kupokea tuzo hiyo.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZAMANI WA BOTSWANA, KETUMILE MASIRE AMEFARIKI DUNIA

Sir Ketumile Masire enzi za uhai wake

Rais wa zamani wa Botswana, Sir Ketumile Masire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.

Taarifa zilizotolewa zinasema Sir Masire alifariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali alikokuwa amelazwa toka wiki iliyopita.

Sir Ketumile Masire alikuwa Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1980 hadi 1998 na enzi za uhai wake aliongoza juhudi mbalimbali Barani Afrika ikiwa ni pamoja kuongoza tume iliyochunguza mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Waziri Mahiga akutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo alipokutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore yenye Makao Makuu Jijini Arusha,Tanzania. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe. Wiziri Mahiga mjini Dodoma, wamejadili masuala mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya mahakama hiyo ikiwemo majengo ya ofisi ili kuiongezea ufanisi zaidi. 
Mazungumzo yakiendelea; Kushoto ni Wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na kulia kwa Rais wa Mahakama, ni Mtumishi wa Wizara Bw. Beatus Kalumuna 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore mara baada ya mazungumzo 

Picha ya Pamoja 
Waziri Mhe. Mahiga akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo 
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo 

MAHAKAMA KUU YA ZIMBAMBWE YAPIGA MARUFUKU WATOTO KUPIGWA


Mahakama Kuu nchini Zimbabwe imepiga marufuku kitendo cha kuwapiga watoto mashuleni na hata majumbani nchini humo.

Uamuzi huo wa Mahakama umetolewa kufuatia mzazi mmoja kulalamika mtoto wake darasa la kwanza mwenye miaka 6 kupata michubuko baada ya kuchapwa na mwalimu.


Mzazi Linah Pfungwa amesema mtoto wake wa kike alipigwa na mwalimu kwa kusahau kitabu chake kusainiwa na mzazi kuthibitisha amefanya kazi aliyopatiwa kuifanya nyumbani.

NAIBU KATIBU MKUU- NISHATI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA MAFUTA KONGO


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia mbele) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kalemie, Kongo kwa ajili  ya kushiriki mkutano  wa kubadilishana data na uzoefu kuhusu mafuta katika Tanganyika uliofanyika hivi karibuni nchini Kongo. Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Burundi, Kongo na  Zambia. Wengine kutoka kushoto ni  Gavana wa Jimbo la  Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala, Waziri wa Migodi na Madini Nchini Zambia, Chris Yaluma na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) na Gavana wa Jimbo la  Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria, Wizara ya Nishati na Madini, Anna Ngowi (kushoto) pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Marais wa wa mataifa mbalimbali katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Abba nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU

KIMBUNGA CHAKATISHA HOTUBA YA ZUMA BAADA YA HEMA KUANGUKA

 
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelazimika kukimbia kuokoa maisha yake baada ya hema alilokuwa akitumia kutoa hotuba kuanguka.

Kimbunga hicho kilichoambatana na mvua kililichana na kuliangusha hema hilo ambalo rais Zuma alikuwa akitoa hotuba katika Siku ya Upatanishi.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya jamii inaonyesha watu wakihaha kusalimisha maisha yao wakati hema hilo likipeperushwa juu na upepo, na rais Zuma kukimbizwa sehemu salama.

Hakuna taarifa za awali zilizopatikana iwapo kulikuwapo na watu waliojeruhiwa wakati wa kimbunga hicho huko Gopane nchini Afrika Kusini.

MSAKO WA MAJAJI WALARUSHWA WAFANIKIWA KUKAMATA DOLA LAKI 8 NIGERIA

Vikosi vya usalama vya Nigeria vimekamata fedha kiasi cha dola 800,000 katika msako uliofanywa kwenye nyumba za majaji wa nchi hiyo wanaoshukiwa kuwa ni wala rushwa.

Wakala wa taasisi ya DSS umesema msako huo umefanyika katika siku za hivi karibuni na tayari majaji kadhaa wanashikiliwa.

Tangu aingie madarakani rais, Muhammadu Buhari, aliahidi kukabiliana na matukio ya rushwa nchini Nigeria.

REGIONAL HEALTH FORUM PARTICIPANTS CALL FOR NEW MEASURES TO REDUCE HARMFUL NON-COMMUNICABLE DISEASES ACROSS AFRICA AND THE MIDDLE EAST

Prof. Dr. A. Sameh Farid, Founder and President, New Giza University & Former Minister of Health, Egypt, Amadou Mahtar Ba, Founder, All Africa and Prof. Barthelemy Nyasse, University of Bamenda, Cameroon

LONDON, United Kingdom, 09 October 2016,-/African Media Agency (AMA)/- Scientists, healthcare providers, policymakers and private sector companies met in Dubai for the first ever Middle East and Africa (MEA) Health Forum on 'Harm Reduction for Healthier Societies'. With a focus on obesity and tobacco, participants at the inaugural forum considered some of the major developments and transformative innovations being adopted to help build healthier societies in these regions.

Panelists and speakers discussed how potentially preventable risk factors such as poor diets, high blood pressure, high body mass index (an indicator of obesity and being overweight), and smoking are contributing to the growing burden of non-communicable diseases in the MEA region. There are 1.4bn smokers on the planet today and 1.4bn deemed overweight. These numbers are of crisis proportions. As these non-communicable diseases (NCDs) are looming as the greater threat, forum attendees recommended that existing public health policies and strategies be revisited in order to allow the formulation of new, evidence-based measures for harm reduction. They held that such measures including smarter policies based on ongoing robust scientific research.

Dr Nasim Ashraf, CEO of the DNA HealthCorp, noted that for the first time in the history of humanity, the new generation of children, the millennials, will be worse off economically and also from a health perspective. And for this to change the whole system needs to change, which is too often skewed towards treatment rather than prevention.

In the final remarks summarising proceedings from the discussions there was a consensus that harm reduction should be part of any effective public health strategy in national efforts to lower the health burden associated with smoking and the overconsumption of sugar, saying that these two health issues are widely acknowledged as a leading cause of NCDs.


Novel products such as vaping, for example, were 95% less toxic than traditional cigarettes and could simply not be discarded in policy formulation. At the same time, obesity should not be looked at in isolation. Sleep deprivation for example is a contributing factor to an unhealthier lifestyle.

Too often policy makers, scientists and industry are working in isolation when they needed to collaborate and engage more closely to develop better solutions.

In its summary the forum called for more alternatives and innovative solutions, including the establishment of an independent research fund or institution to research, evaluate and develop solutions in the area of tobacco.

On sugar harm reduction, the Forum noted a consensus that sugar in itself is not harmful when consumed in appropriate quantities. However, the Forum called for the establishment of mechanisms to identify instruments and published studies on health risks associated with the use of sugar in all its forms, broader public health awareness programmes on this issue and smarter regulation when it comes to acceptable sugar levels in consumer products.

Distributed by African Media Agency (AMA) on behalf of IC Publications.

ASKOFU TUTU ABAINISHA UWEZEKANO WA KUOMBA KUSAIDIWA KUFA

Askofu Dedmond Tutu wa Afrika Kusini amebainisha kuwa anataka kuwa na fursa ya kuomba kusaidiwa kufa.

Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi, amesema hataki kulazimishwa kuendelea kuishi kwa gharama zozote.

Matamshi hayo ya Tutu yameandikwa na yeye katika gazeti la Washghton Post wakati akitimiza miaka 85 ya kuzaliwa.

Mnamo mwaka 2014 Askofu Tutu alibainisha kuwa anaunga mkono wagonjwa mahututi kusaidiwa kufa, lakini alikuwa hajaeleza iwapo yeye pia angependa kusaidiwa kufa.

Mwezi uliopita Askofu Tutu alikuwa amelazwa na kufanyiwa upasuaji ili kumtibu maambukizi ambayo yamekuwa yakijirudia rudia.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI LUSAKA,ZAMBIA

Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe Grace Mujuma akiwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe Judith  Kapijimpanga wakifurahia wakati ndege iliyomchukua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ilipotua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu  Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   akipokea heshima mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka

RAIS ROBERT MUGAME AWANANGA WANAOMZUSHIA KIFO KWA KUWAAMBIA ALIKUFA NA KUFUFUKA

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekebehi uvumi wa hivi karibuni kuhusu afya yake, kwa kusema kwa mzaha kwamba alikufa na kisha kufufuka.

Mugabe, 92, ametoa kauli hiyo ya mzaha, wakati alipowasili kutoka nje katika uwanja wa ndege wa Harare akiwa kwenye hali ya uchangamfu wakati akishuka kwenye ndege.

Safari yake ya ndege ilikuwa ielekea Asia ya Mashariki, lakini badala yake alienda Dubai, ambapo amesema alienda huku kwa masuala ya kifamilia.

Mwezi Mei, mwaka huu mke wa rais Mugabe, Grace alisema kuwa rais huyo ataiongoza Zimbabwe hata akiwa kaburini.

UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU ZAMBIA WAANZA HUKU KUKIWA NA ULINZI MKALI

Zoezi la upigaji kura za urais na ubunge limeanza nchini Zambia baada ya kumalizika kwa kampeni zilizokabiliwa na mapambano baina ya wafuasi wa vyama vinavyokinzana.

Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa ni wa upinzani mkali baina ya rais Edgar Lungu wa chama cha PF na mgombea wa upinzani wa chama cha UPND, Hakainde Hichilema.

Kwa mara ya kwanza, mgombea wa urais nchini humo atalazimika kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, ili kuepuka uchaguzi wa marudio.
                        Rais Edger Lungu akihutubia katika moja ya mikutano ya kampeni
                             Mgombea urais wa chama cha upinzani Hakainde Hichilema

Mjue Kiundani 'Simba wa Afrika' Robert Mugabe

Na Geofrey Chambua
1. Mzaliwa wa Februari 21. 1924; Komredi Robert Gabriel Mugabe Ni mtoto pekee aliyesalia katika familia yao kwani kaka zake wawili walifariki akingali mdogo sana na baba yake alitelekeza familia yao mnamo mwaka 1934 na kumlazimu mama yake kuolewa na mwanaume mwingine. Ingawa unamjua Mugabe kama Rais wa Zimbabwe ukweli ni kwamba Baba yake mzazi Gabriel Matibili ni Mmalawi aliyekua fundi seremala ila mama yake ambaye ndiye aliyemlea ni Mshona wa Zimbabwe kwa asili. 

2. Kwa miaka 92 amekua​ akitumia zaidi vyakula vya asili ya mimea (Vegetarian) chakula chake kikuu ikiwa ni maboga ingawa aghalabu hula nyama pori na hasa nyama ya ​S​imba na ​T​embo. Mugabe pia hatumii kileo wala kuvuta sigara

3. Huamka saa kumi alfajiri kila siku kwa mazoezi mepesi na hupenda sana kusikiliza BBC baada ya hapo, huenda hii ikaelezea kwa nini husinzia sana hata kwenye hadhara
4. Ana jumla ya shahada SABA. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika ​C​huo ​K​ikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine sita kwa njia ya masafa (Distance Learning) kati ya hizo mbili ​za Sheria ​akiwa gerezani. Kazi yake ya kwanza kabla ya kujiunga na siasa ni UALIMU na alianza kufundisha Chuo cha Ualimu Chalimbana nchini Northen Rhodesia (Zambia kwa sasa) kisha Apowa Sekondary nchini Ghana. Mugabe amekua akisisitiza sana katika elimu nchini mwake na ameiwezesha Zimbabwe kuweka rekodi ya juu ya kufuta ujinga Afrika kwa 90%. Mnamo Mwaka 2005 alitunukiwa shahada ya heshima ya Uprofesa na Chuo Kikuu cha Diplomasia huko China kwa uwezo wake wa kusomea karibu fani zote muhimu duniani ikiwemo sheria, uchumi, historia, sayansi, sanaa, utawala na elimu.......yasemekeana rafiki mkubwa wa maisha ya Mugabe ​tangu utotoni ​ ​​ni 'Kitabu kwa sana'​ ​ 

5. ​Upande wa michezo, ​Hupendelea sana Kriketi na Kisoka yeye ni mnazi wa Chelsea ya Uingereza na Barcelona kwa Upande wa Spain na yasemekana ana mizuka sanaya kisoka pia ...... 'Huwa nina midadi sana ninapotazama kandanda, 'wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwa kupiga mateke chochote kilicho mbele yangu”

6. Mugabe pia ni mcheza kamari maarufu (kubeti) ingawa kisiri sana kwani mwaka 2000 alistua wengi aliposhinda ZimDola 100,000 kwenye Bahati Nasibu iliyoendeshwa na Benki ya Biashara (ZimBank)
7. Mtoto wake wa tatu alimpata mwaka 1997 wakati huo Bob akiwa na miaka 73 alizaa na aliyekua karani muhtasi wake aitwaye Grace Marufu (miaka 38) ambaye kwa wakati huo alikua mke wa mtu (mchepuko) na akalazimika kumtaifisha kama mkewe wa TATU katika maisha yake ya ndoa

8. Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-Bob haamini sana katika ufuasi wa dini. Alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, Jongwe huyu wa Afrika alikiri kwamba hata maswahiba wake wengi humchukulia Mugabe kama mpagani tu kutokana na mtindo wa maisha yake (life style)​.

9. Tayari ameshaweka wazi nia yake ya kuwania kiti cha Uraisi mnamo mwaka 2018 ​ambapo ​panapo majaliwa atakua na miaka 94 hivyo atakua ametimiza miaka 30 ya uraisi iliyotanguliwa na miaka 7 ya Uwaziri Mkuu (The oldest and longest serving President in the whole world)
Al​iwahi kuulizwa n​a waandishi wa habari 

​Mwandishi: Mr President, When will you say goodbye to the people of Zimbabwe? (Lini utawaambia kwa heri wananchi wa Zimbabwe?)

Mugabe: Where are they going? (Kwani wanaenda wapi?)​
10. Mugabe ambaye hujulikana sana kwa majibu na misemo yenye utata sana hasa kwa waandishi wa habari, amewahi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha wateule wachache wa kuwania tuzo ya amani ya Nobel ingawa hakushinda kufuatia mfululizo wa mauaji nchini kwake kipindi hicho baada ya kumtimua Joshua Nkomo kutoka Baraza lake la ​Ma​waziri hali iliyowachukiza Wandebele na kuzua mapigano ya kimbari dhidi ya Washona.
11. Mugabe amejipatia umaarufu Barani Afrika na Kwingineko Duniani kwa misimamo yake thabiti kiasi cha kuitwa dikteta wa aina yake (In 2007, Parade magazine ranked Mugabe the 7th worst dictator in the world) na hasa kupinga ukoloni mamboleo nchini mwake na pia tabia za kushiriki mapenzi ya jinsi moja ambapo mnamo mwaka 1997 Maha​ka​ma​ ​ya nchi hiyo ilimtia hatiani kwa makosa 11 mtangulizi wake Cannan Banana kwa kushiriki ngono kinyume cha maumbile (sodomy). Banana ndiye Rais wa Kwanza wa Zimbabwe.


12. Mnamo mwaka 1975, Mugabe alichaguliwa kuwa Rais wa ZANU-PF huku akingali anatumikia kifungo kwa chagizo kubwa la Askofu Abel Muzorewa 

Mugabe ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimia umri wa miaka 92 mwaka huu na tayari Chuo kimoja cha utafiti nchini Uingereza kimetaarifu Mugabe kuishi milele kutokana na mwili wake kuwa na vinasaba ambavyo havina urafiki na mauti licha ya kuzushiwa kifo mara kadhaa. 
Mnamo Februari 16 mwaka huu alinukuliwa akisema kwamba hana mpango wa kustaafu URAIS hadi 'Mwenyezi Mungu atakapomuita' 

Mwandishi: Mweshimiwa Rais, huoni kwa umri wako wa miaka 89 ni wakati mwafaka wa kupumzika na kuachana na kazi?

Mugabe: Umewahi kujaribu kumwuliza swali hili Malkia Elizabeth au swali lako ni kwa ajili ya viongozi wa Kiafrika tu?

MCHUNGAJI WA ZIMBABWE ALIYESHIKILIWA KWA KUITISHA MGOMO WA KITAIFA ATOA WITO MGOMO UENDELEE

Mchungaji nchini Zimbabwe aliyekamatwa kwa muda baada ya kuratibu mgomo wa kitaifa wiki iliyopita ametoa wito kwa watu kuendelea kugoma.

Mchungaji Evan Mawarire ameiambia BBC kuwa watu wanapaswa kuendelea kukaa nyumbani, kama njia ya kampeni dhidi ya rushwa, uchumi mbovu na ukosefu wa ajira.
Mchungaji Mawarire ambaye aliachiwa jana na mahakama baada ya kutupilia mbali mashtaka yake, amesema kampeni hiyo imejidhatiti kuleta mabadiliko nchini humo.

Migogoro ni chanzo cha kudidimia kwa Uchumi wa Afrika


Benjamin Sawe -Maelezo
Dar es Salaam

Amani ni msingi wa maendeleo na hivyo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.Bila amani,nchi haiwezi kufanya shughuli za maendeleo hata pale ambapo maendeleo yameshapatikana,huweza kuvurugwa endapo amani itatoweke katika nchi.

Nchi ambazo kwa miaka ya hivi karibuni zimejitaidi kupiga hatua za maendeleo na zinaendelea kufanya jitiada kuhakikisha kuwa zinapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kwa faida ya wananchi wote,jitiada hizo pia,kwa baadhi ya nchi zimeathiriwa na migogoro.

Matokeo ya migogoro hiyo ni mamilioni ya waafrika wasio na hatia kupoteza maisha yao na mamilioni zaidi kujeruhiwa.Pia mamilioni ya wanawake na watoto kupatwa shida kubwa na baadhi ya watu kukimbia nchi zao na kukimbilia nchi za jirani katika kuokoa maisha yao hivyo kujikuta wakiishi maisha ya dhiki nje ya nchi yao.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2009,Afrika ilikuwa na wakimbizi milioni 3 ambayo ni asilimia 20 ya wakimbizi wapatao milioni 10.5 duniani.Aidha,Afrika inakisiwa kuwa ina watu milioni kumi na mojana laki sita ambao wamelezimika kuhama makazi yao kwa ajili ya vita

Migogoro migogoro huwa kikwazo kikubwa cha shughuli za maendeleo siyo tu kwa watu binafsi bali pia kwa taifa.Fedha ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye huduma muhimu ya jamii kama afya,elimu,maji ni fedha ambazo huelekezwa katika manunuzi ya silaa.

Inakadiriwa kuwa hasara ya kiuchumi inakadiriwa kuwa wastani wa dola bilioni kumi na nane kwa kila mwaka sababu ya migogoro.

Hali hii ya migogoro katika bara la Afrika imelifanya bara hili kujulikana kama bara la mapigano jambo ambalo ni dhahiri linasikitisha hivyo hatuna budi kuondokana na hali hiyo ya migogoro na kuwa bara huru lisilo na migogoro.

Ni kweli kuwa katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko,kutokana na juhudi zilizofanyika,Afrika imefanikiwa kupunguza idadi ya migogoro kuliko ilivyokuwa katika miaka ya 1980 wakati ambapo nchi nyingi zilikuwa na migogoro

Mfano nhci kama Liberia,Sierra Leone,Msumbiji,Angolo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Burundi na Comoro nazo zimeendelea kuimarisha amani,Hali hii inatupa faraja lakini bado Bara la Afrika linamigogoro kama vile ya Somalia na Darfur kuko Sudani.

Mgogoro wa Somalia ni mgogoro wa muda mrefu sasa ambao ni changamoto kubwa kwa bara la Afrika na jamii ya Kimataifa kwa ujumla na hivyo unahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Hali ya usalama nchini Somalia ambayo kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha ambapo kwa ujumla usalama wa wananchi wan chi hiyo umo katika hali ya hatihati.

Kwa upande Tanzania tunafahari kubwa ya kuwa mstari wa mbele katika kujenga mazingira yetu wenyewe ya kuwa na amani,utulivu na mshikamano na pia katika kusaidia ndugu na majirani zetu na sehemu nyingine za Bara la Afrika katika kufanukisha lengo la kuleta amani popote pale inapokosekana.

Sote tunatambua kuwa Serikali ya Tanzania katika kutetea amani katika bara la Afrika imepeleka vijana wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) katika miaka ya nyuma walikwenda nchini Liberia kwa lengo hilo.Na hivi karibuni wanajeshi wetu wamekwenda Darfur kuungana na wanajeshi wengine wa Kiafrika na nchi nyingine chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Vilevile,viongozi wetu wa Afrika wameshiriki na wanaendelea kushiriki kutoa michango yao muhimu katika juhudi juhudi za kuleta amani.

Mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa jakaya Kikwete ametoa mchango muhimu katika kumaliza mgogoro wa ndugu zetu wa Kenya uliotokana na uchaguzi uliofanyika nchini humo mwaka 2007.

Pia Rais mstaafu wa awamu ya tatu,Mheshimiwa Benjamin Mkapa ametoa na anaendela kutoa mchango wake katika juhudi za kurudisha amani na utulivu huko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hasa mgogoro w mashariki ya Kongo.

Mkapa anazitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhakikisha nazo zinaendelea kusaidia nchi ya Burundi ili amani ipatikane.

Anasema wenye jukumu la kuleta amani kwa nchi yao ni Warundi wenyewe na kuwataka kukaa meza moja ili kujadiliana pamoja na kuondoa tofauti zao na amani ni kitu muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Burundi, hivyo ni vyema wakatumia mkutano huo vizuri kufikia muafaka.

Mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa, Balozi Roeland Van der Geer akizungumza kwa niaba ya jumuiya hiyo anasema nchi ya Burundi inatakiwa kuhakikisha amani inapatikana ili kuhakikisha kila raia wa nchi hiyo anapata maendeleo.

Aidha mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika katika nchi za Maziwa Makuu, Balozi James Benomaar alisema jumuiya hiyo ina imani kubwa na Rais Mkapa katika kusuluhisha mgogoro huo na kutoa rai kwa Warundi kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa nchi yao ili kupunguza wimbi la wakimbizi wanaokimbilia nchi mbalimbali kwa usalama wa maisha yao.

Inasikitisha kuona bara letu la Afrika kutangazwa kama ni bara la mapigano hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa amani yetu inaendela kudumu na kuhakikisha amani yetu inaendelea kulindwa na inapatikana katika maeneo mengine barani Afrika.

MCHEZAJI SAMUEL ETO'O AAGA KAMBI YA UKAPERA

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Chelsea mshambuliaji Samuel Eto'o amefunga ndoa jana na mpenzi wake wa muda mrefu Georgette Tra Lou na kufanya bonge la sherehe.

Ndoa ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, imefungwa huko Stezzano, Italia, huku mamia wakikusanyika kumuona Eto'o na mkewe nje ya kanisa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye alicheza misimu miwili Serie A akiwa na Inter Milan balikuwa amevalia suti yenye rangi ya kijivu, alifika kanisani akiwa kwenye gari la Vintage.
                                Samuel Eto'o akifunga ndoa kanisani na Georgette Tra Lou
                              Mke wa Samuel Eto'o Georgette Tra Lou akifurahi ndoa yake
Asanteni kwa kuja:  Samuel Eto'o akipunga mkono kuwashukuru watu walikuja kushuhudia ndoa yake