MCHEZAJI SAMUEL ETO'O AAGA KAMBI YA UKAPERA

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Chelsea mshambuliaji Samuel Eto'o amefunga ndoa jana na mpenzi wake wa muda mrefu Georgette Tra Lou na kufanya bonge la sherehe.

Ndoa ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, imefungwa huko Stezzano, Italia, huku mamia wakikusanyika kumuona Eto'o na mkewe nje ya kanisa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye alicheza misimu miwili Serie A akiwa na Inter Milan balikuwa amevalia suti yenye rangi ya kijivu, alifika kanisani akiwa kwenye gari la Vintage.
                                Samuel Eto'o akifunga ndoa kanisani na Georgette Tra Lou
                              Mke wa Samuel Eto'o Georgette Tra Lou akifurahi ndoa yake
Asanteni kwa kuja:  Samuel Eto'o akipunga mkono kuwashukuru watu walikuja kushuhudia ndoa yake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni