Bodi ya Utalii Tanzania
imeanzisha touvuti maalumu iitwayo Destination Tourism Portal pamoja na
nyenzo (App) kwa watumiaji wa simu za mikononi na hivyo kuendelea
kujikita zaidi katika matumizi ya tovuti na mitandao ya Kijamii
(e-marketing) katika kutekeleza majukumu yake ya utangazaji wa vivutio
vya Utalii vya Tanzania duniani kwa lengo la kuvutia watalii wengi
zaidi.
“Tovuti hii inalenga zaidi katika
kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta ya utalii
kufanya biashara zao kwa urahisi na kukuza mapato yao na faida zaidi”
alisema Bw. Chitaunga.
Ameongeza kuwa Tovuti hii inatumia anuani ya www.tanzaniatourism.com ina taarifa nyingi sana za
vivutio vya utalii
vinavyopatikana hapa nchini lakini pia taarifa kuhusu malazi
(accommodation) na huduma nyinginezo na kwamba inamwezesha mtalii
kufanya malipo online.
Mkurugenzi huyo wa Masoko amesema
kuwa sambamba na uanzishaji wa tovuti hiyo, tumeanzisha pia nyenzo
rasmi ya Utalii iitwayo Tanzania Tourism App ambayo kama ilivyo kwa
portal ina taarifa nyingi za utalii ikiwa ni pamoja na vivutio vya
utalii, malazi na namna ya kupanga safari kwa mtalii anayetaka
kutembelea Tanzania, na kufanya malipo online.
Amesema kuwa Nyenzo (App) hii
inapatikana katika Google play store kwa watumiaji wa simu za Android
duniani kote na muda si mrefu itapatikana pia katika AppStore kwa
watumiaji wa simu za Iphone.
Amedokea kuwa zipo nyenzo (Apps)
kadhaa zilizoanzishwa na makapuni au watu binafsi kama vile Tanzania
Safari Guide; Tanzania Travel Safari; Destination Tanzania: Tanzania
Travel and Tourism n.k lakini hii ya kwetu ndiyo hasa rasmi ya Serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni