MWANAMKE MDACHI ALIYEDAI KUBAKWA QATAR AHUKUMIWA KWA KUFANYA NGONO NJE YA NDOA

Mahakama nchini Qatar imemtia hatiani mwanamke mmoja Mdachi, kwa kufanya ngono bila ya kuolewa baada ya kuwaambia polisi wa nchi hiyo amebakwa.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22, amehukumiwa kifungo cha nje na amepigwa faini ya dola 824, na pia atalazimika kuondoka Qatar kwa nguvu.

Wakili wake amesema mteja wake alikunywa pombe akiwa hotelini Doha mwezi Machi na kuamka asubuhi akajikuta kwenye ghorofa asilolitambua na ndipo alipobaini kuwa kabakwa.

Mtuhumiwa wa ubakaji alyedai waliridhiana kufanya ngono, amehukumiwa kupigwa bakora 100, kwa kufanya ngono nje ya ndoa. Pia atachapwa fimbo 40 kwa kunywa pombe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni