Mike
Tyson na Floyd Mayweather ni miongoni mwa mabondia wa zamani maarufu
waliotoa salamu za rambirambi kwa kifo cha bondia mkongwe na maarufu
duniani Muhammed Ali katika mitandao ya kijamii, katika kuguswa na
kifo cha bingwa huyo mara tatu wa uzito wa juu.
Ali
amefariki dunia leo asubuhi huko Arizona akiwa na umri wa miaka 74,
kutokana na tatizo la mfumo wa pumzi, baada ya kumudu kupambana na
ugonjwa wa kutetemeka viungo vya mwili na kushindwa kuongea vizuri
uitwao Parkinson aliodumu nao kwa muda wa miaka 32.
Salamu
za rambirambi kuanzia kwa nyota wa michezo hadi rais Barack Obama
zimekuwa zikimiminika kutoka kila ya pande duniani, katika kumuelezea
Ali ambaye alipachikwa jina la bondia bora kuliko waote kutokana na
mafanikio yake akiwa ulingoni na kuwavutia mamilioni ya watu duniani.
Gwiji la Soka Pele akimkumbatia Muhammed Ali hii ilikuwa mwaka 1977 Jijini New York Marekani
Rais Barack Obama akitoa ujumbe wa rambirambi ulioambatana na picha katika mitandao ya jamii
Bondia Muhammed Ali akiwa ameshamdunda kwa KO George Foreman katika pambano lililopewa jina la Rumble in the Jungle
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni