MKOA
wa Arusha, utaadhimisha siku ya mazingira duniani June 5 kwa kupanda
miti aina mbalimbali ya matunda ,vivuli na ya asili kwenye shule za
msingi na vyanzo vya maji ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Katibu tawala mkoa wa
Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele
chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote
ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na
kutekeleza jukumu la shirika la mazingira duniani, UNEP.
Amesema shirika la umoja wa
mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya
maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na
kusimamia mazingira yao.
Alisema kila nchi mwanachama
ikiwemo Tanzania, inayo sauti katika kikao cha baraza la mazingira
duniani juu ya mazingira endelevu .
Kwitega,alisema mwaka huu 2016
maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa
na kauli mbiu isemayo uvumilivu ufike mwisho juu ya biashara haramu ya
wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
Alisema kaulimbiu hiyo inatutaka kuacha kuwauwa wanyamapori kwa lengo la kuuza viungo vyao na kuharibu mazingira .
Kwitega,amesema katika
kutekeleza jukumu hilo mkoa huo, unashirikiana na wadau mbalimbali wa
maendeleo zikiwemo halmashauri na asasi binafsi kuadhimisha siku hiyo ya
mzngira duniani kwa kupanda miti maeneo mbalimbali.
Alisema kwa kuanza mkoa
utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha,
ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye
chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili ambayo ni rafiki
wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
Alisema maadhimisho hay mwaka
huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la
kuadimisha maadhimisho hayo kwa kushirikiana na halmashauri zake na
wadau wake wa maendeleo.
Alisema kauli mbiu ya taifa
mwaka huu inasema tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu
na mkoa utaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii
kuanzia juni 2 hadi siku ya kilele juni 5
Kwitega, alisema katika
maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya
kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na
taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema kuwa siku ya kilele ya
maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye
bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni