Balozi
wa India hapa nchini, Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya watanzania wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi
siku ya Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Coco beach jijini Dar es
Salaam.
Balozi
wa India hapa nchini, Sandeep Arya akiwaonesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) nembo ya Yonga, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliofika kufanya mazowezi ya Yoga, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
MAZOEZI
ya viungo vya mwili yenye asili ya Indi nchiniIndia yanatarajia
kufanyika Juni 19 mwaka huu katika viwanja vya ufukwe wa Cocobeach
jijini Dar es Salaa ikiwa ni kuadhimisha siku ya Utamaduni wao na
kimataifa kwa ujumla.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam, Balozi wa India hapa nchini,
Sandeep Arya amesema kuwa Yogo ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye
asili katika falsafa ya uhindi kwa mda wa miaka mingi.
Alimnukuu
Waziri Mkuu wa India, Shri Narendra wakati akihutubia mkutano wake wa
69 wa Baraza Kuu la Umojawa Mataifa Septemba 27, 2014 alipendekeza
jumuiya yakimataifa kupitisha siku ya Kimataifa ya Yoga.
Aidha
ameeleza kuwa siku ya Yoga sio tu kufanya mazoezi bali mbinu ya
kujitambua na kutambua mahusiano ya mtu na dunia na mazingira yake.
Balozi
huyo amewaomba watanzania kujitokeza kwawingi kufanya mazoezi siku ya
Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Cocobeach Dar es Salaam huku
akisemamazoezi ni uhai wa binadamu hivyo siku hiyo watawezakufundishwa
mbinu mbalimbali za kufanya mazoezi yaviungo kutoka kwa wataalamu kutoka
nchini India.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni