Na Mahmoud Ahmad Arusha
Taifa
letu linahitajia kuangalia kwa mapana takwimu za wahitimu wahandisi ni
wengi kuliko wahitimu mafundi sanifu kutokana na hali hiyo huduma za
kihandisi na za ufundi hazitakidhi matakwa ya maendeleo yanayotarajiwa
na itakuwa vigumu kufikia malengo makuu ya dira ya maendeleo ya Tanzania
2025 na pia ya MKUKUTA awamu ya pili.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi
Maimuna Tarishi kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo Prof Joyce Ndalichako
wakati wa uzinduzi wa maabara ya skimu ya umwagiliaji (Hydraulics
Engineering) iliyojengwa na shirika la misaada la Japan(JAICA)kwenye
chuo cha ufundi Arusha jijini Arusha.
Alitanabaisha
kuwa Mashirika ya kimataifa yamekuwa kupendekeza kuwa na uwiano kwa
kila mhandisi mmoja pawepo na mafundi watano na mchundo 25 ilikuweza
kuleta maendeleo ipasavyoi katika nchi yetu.
Tarishi
alisema kuwa kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini ni ndogo
kwa sababu ya uhaba wa maofisa ugani na wataalamu mbali mbali wa
umwagiliaji wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji hasa kwenye ngazi ya
halmashauri zetu hapa nchini,chuo kama sehemu inatakiwa kubuni mbinu
mbadala za kuweza kutowa na kuandaa mipango ya masomo yatakayosaidi
upatikanaji wa ajira kwenye soko la ajira.
"Changamoto
ya kupata ajira kwa baadhi ya waajiri hawajajumuisha hii kada ya
uhandisi ujenzi na umwagiliaji katika(Scheme of service) zao hivyo basi
tunaomba waajiri wote kujumuisha kada hii muhimu katika(Scheme of
service)zao ili kutatua changamoto hii na kuongeza tija katika kazi zetu
za kilimo cha umwagiliaji"alisema Tarishi
Aidha
katibu mkuu huyo alitanabaisha kuwa kutokana na hali hiyo tunaomba kuwa
program za ufundi sanifu zipewe kipaumbele kwani taifa lenye rasilimali
nyingi litanufaidika na rasilimali hizo tu iwapo litaziongezea
thamani(processing and value addition)kabla ya kuuzwa vinginevyo taifa
hilo litachuuza hizo rasilimali na halitaendelea.kwani mafundi saniu
mahiri ni mhimili mkuu wa kuongeza thamani ya rasilimali zetu.
Kwa
upande wake balozi wa japani hapa nchini Masaharu Yoshinda wakati
akikabidhi mradi huo kwa serikali ya Tanzania alisema kuwa mradi huo wa
mashine ya umwagiliaji ni mkubwa na mashine ya aina hiyo haipo katika
ukanda huu wa Afrika mashariki na kati na itasaidia nchi ya Tanzania
kuwajenga wataalamu wa masuala ya umwagiliaji na kukuza kilimo cha
umwagiliaji nchini kwenu.
Alisema
kuwa serikali ya Japan itaendelea kutoa wataalam katika kuhakikisha
utaalamu huo unawafikia watanzania wote ilikukuza uchumi wa nchi yenu
kwa kuweza kukuza uzalishaji na hatimaye viwanda.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Arusha dkta Richard Masika alisema
kuwa mradi huo utasaidia chuo na vyuo vyengine kuweza kuinua taaluma
kwani mashine hiyo itasaidia kukuza na kuweka mezania kwa wahitimi na
kwenda kufanya vizuri katika kukuza kilimo cha umwagiliaji hapa nchini.
Alisema
kuwa serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele katika kujengea uwezo
chuo kupitia ufadhili wa mfuko wa chakula wa pamoja kati ya Tanzania na
Japan(TJFACF) Kwa wanachuo na chuo wamejengewa uwezo wa kufundisha
program ya uhandisi ujenzi na umwagiliaji kupitia mradi"kujenga uwezo wa
wanataaluma katika kutoa mafunzo ya uhandisi Umwagiliaji yaani (ATC
irrigation human Resoursces Development Programme AIHRDP)Unaofadhiliwa
na serikali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni