MTOTO MTUKUTU ALIYETELEKEZWA MSITUNI NA WAZAZI WAKE NCHINI JAPAN APATIKANA

Mtoto wa kiume aliyepotea eneo la msitu nchini Japan tangu jumamosi baada ya kuachwa na wazazi wake kama adhabu, amepatikana akiwa hai.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba aitwae, Yamato Tanooka, amekutwa kwenye kambi ya jeshi karibu na Shikabe kaskazini mwa Hokkaido, kilomita chache kutoka alipoachwa na wazazi wake.

Wazazi wake awali walisema mtoto huyo amepotea, lakini baadaYe walikiri walimtelekeza kama adhabu kwa kuwa ni mtukutu.
   Mwanajeshi akionyesha magodoro aliyokuwa akilalia mtoto huyo kwenye kambi ya jeshi 
Baba wa mtoto huyo Tamayuki Tanooka akiomba msamaha kwa kitendo chake cha ukatili dhidi ya mtoto wake
                          Muonekano wa kambi ya jeshi ambayo mtoto huyo alipatikana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni