Mratibu
 wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza 
Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison 
Chinyuka akizungumza na Viongozi wa vikundi vya mradi huo (hawapo 
pichani) walipotembelea Kata ya Makanya Wilaya ya Same kukagua 
utekelezaji wa mradi huo Juni 14, 2016.
Afisa 
Mtendaji Kata ya Makanya Bw.Josephat Kitunga akiwasilisha taarifa ya 
utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza 
Athari za Maafa katika Kata yake alipotembelewa na Wataalamu wa masuala 
ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kukagua miradi inayotekelezwa, tarehe 
14 Juni, 2016.
Mkuu 
wa Wilaya ya Same Mhe.Herman Kapufi (katikati) akizungumza na baadhi ya 
Wadau wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari
 za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame walipotembelea Wilaya 
hiyo kuangalia utekelezaji wa mradi katika kata ya Makanya, Vunte na 
Hedaru Mkoani Kilimanjaro.
Mchumi
 Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Magreth Sembuyagi 
akifafanua jambo walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Same 
Bi. Monica Kwilulihya (hayupo pichani) ili kuendelea na shughuli za 
kukagua miradi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.
Mnufaika
 wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za 
Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bi.Neema akifurahia 
mafanikio ya kununua ng’ombe mara baada ya kuuza kuku aliozalisha 
kupitia mradi huo katika Kata ya Makanya Wilaya ya Same mkoani 
Kilimanjaro, tarehe 14 Juni, 2016.
Mwenyekiti
 wa Kikundi cha Ujamaa Bi. Khadija Mrutu akihudumia mifugo aliyozalisha 
kupitia Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari 
za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame unaoratibiwa na Ofisi ya 
Waziri Mkuu mara baada ya kutembelewa na Wadau wa mradi huo kwa kufanya 
tathimini za utekelezaji wake. 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni