Mkuu
wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda ameyataka mashirika yanahusika
na kutathimini viwango vya ubora nchini kuhakikisha wanafika katika
viwanda na kwa wazalishaji wadogo wadogo ili kuweza kupata twakimu za
ubora kwa usahii zaidi na kuboresha hali za bidhaa hapa nchini
Wito
huo ameutoa hivi karibuni kwenye mkutano wa mashrikia ya viwango
Barani Afrika ambapo shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika
la viwango Afrika ARSO wamezikutanisha nchi zipatazo 15 pamoja na wadau
wengine kutoka mataifa ya Ulaya.
"Ni
jukumu la viwango, unajua mara nyingi tumekuwa na matatizo mengi kwenye
uzalishaji wa bidhaa zetu,kwenda kuwa chini ya viwango,lakini kwa
utaratibhuu ambao (TBS)wameuandaa wao wenyewe,ninauhakika sasa tutakuwa
na vitu vinavyokwenda na viwango,ama kiwango ambacho kipo kwenye
soko,labda niombe (TBS)wawe na wasimamzi ambao wanaweza kuenea Nchi
nzima ili kuhaikisha tupata bidhaa ambazo zipo kwenye viwango,alisema
N'tibenda."
Mkurugenzi
mkuu wa TBS Tanzania Joseph Masikitiko amesema kuwa mkutano huo ambao
wanaanza kukaa kamati kuu ya viwango Afrika na baadae kufuatiwa na
mkutano mkuu wa wanachama wa shirika la Viwango TBS sambamba na kuwepo
na siku ya viwango Afrika.
Aidha
ameongezea kusema kuwa katika mkutano huu Mashirika hayo yanatarajiwa
kukaa na kutoka na maazimio ya pamoja na kupata njia maafaka za kupata
bidhaa zinazolingana kwa viwango ili kuweza kupata bidhaa zinazotoka
afika zenye viwango sawa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni