TBS YATAKIWA KUSHUGHULIKIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZISIZO KIDHI VIWANGO

Mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda amelitaka shirika la viwango(TBS) kushughulikia vipasavyo bidhaa  zinazozalishwa hapa nchini zisizo kidhi viwango vinavyotakiwa ili kuondoa bidhaa  zisizo na ubora.
Ameyasema hayo Jana wakati akifungua Mkutano wa 22 wa maonesho ya viwango barani Afrika yaliyoanza jijini Arusha na kushirikisha nchi zaidi ya 15.

Ntibenda alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la nchini katika suala la uzalishaji wa bidhaa  hivyo ili kuhakikisha   bidhaa  hafifu hazitengenezwi kwa mashirika hayo kuongeza juhudi katika usimamizi.
"Ili kuandokana na bidhaa  zisizokidhi viwango hapa nchini mnatakiwa  kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha bidhaa  hizo hazizalishwa" Alisema Ntibenda.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania Joseph Masikitiko alieleza kuwa pasipo viwango huwezi kufanya biashara yoyote iyostahili kwa kuwa itakuwa  haijathibitishwa  .

Alisema lengo la Mkutano huo ni kuboresha viwango kuwa katika hali ya ubora zaidi na   kwa kiwango kimoja Afrika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni