Katibu
 mkuu wa wizara ya elimu sayansi na teknolojia Maimuna Tarishi amezindua
 maaabara ya kisasa yenye mtambo wa utafiti wa mwendo kasi wa maji kabla
 ya kufanya shughuli za kilimo katika chuo cha ufundi jijini Arusha
Akizundua
 mtambo huo uliogarimu dolla za kimarekani kiasi cha shilingi laki nne, 
Maimuna amewataka wanafunzi wa kozi ya kilimo na umwagiliaji kujifunza 
kilimo cha kisasa kinacho endana na teknolojia ya sasa  
Mkuu
 wa chuo hicho cha ufundi cha Arusha Technical Collage Dokta Richard 
Masika amesema kukamilika kwa mradi huo umepunguza garama kubwa ya 
kuwapeleka wanafunzi na wakufunzi kupata masomo nje ya chuo hicho
Amesema
 kwa saa wanafunzi wa kozi ya umwagiliaji na kilimo watapata fursa ya 
kufanya vizuri katika masomo yao mara baada ya kukamilika kwa maabara ya
 kisasa yenye mtambo wa kupima na kufanya utafiti kabla kilimo
Balozi
 wa japani nchini Tanzania Masaharu Yoshida amesema  nchi ya japani bado
 itaendelea kutoa misaada katika chuo hicho hususani katika kukuza 
kilimo cha kisasa kama alivyo ambiwa na Rais wa Jamuhuri wa Mungano wa 
Tanzania dokta john Pombe Magufuli kuwa nchi ya Tanzania inataji kupiga 
hatua katika kilimo cha kisasa
Makamu
 mkuu wa idara ya uwandisi ujenzi katika chuo icho bwana Faraji Mgania 
ameiyomba wizara ya elimu kutatuwa changamoto kadhaa zinazo ikabili 
maabara hiyo ikiwemo vifaa vya mwendo kazi vya kubana maji katika mtambo
 huo
Mtambo
 huo ulio faziliwa na serikali ya japani ni wa kipee barani afrika na 
utasaidia wananfunzi wa chuo icho pamoja na nje ya taasisi hiyo kupata 
mafunzo ya utafiti mwendo.kasi wa maji bila ya kilimo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni