Mvua za msimu zinazonyesha
zikiambatana na radi zimesababisha usumbufu leo asubuhi wakati wa
zoezi la kura ya maoni ya kujiondoa Umoja wa Ulaya likifanyika huku
mafuriko yakitokea katika sehemu ya Jiji la London na Kusini
Mashariki mwa Uingereza.
Baadhi ya barabara za Jiji la London
zimeelezewa kuwa zimegeuka kuwa kama mabwawa ya kuogelea kutokana na
mafuriko hayo, huku usafiri wa reli ya aridhini ukitatizwa na hali
hiyo mbaya ya hewa.
Mtu akiwa ametoka kwenye gari lake kunusuru maisha yake baada ya kuingia kwenye maji
Watu wakiokolewa kwa kutumia boti ya kujaza upepo kutoka maeneo yaliyozingirwa na maji
Abiria wa usafiri wa treni ya aridhini wakiwa wamekwama kutokana na mvua iliyosababisha mafuriko
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni