Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akipata maelezo mara baada ya
kuwasili kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Kutoka
kushoto ni Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa, Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama pamoja na Mkuu wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali, Elias Athanas wakitoa heshima kwa
wimbo wa taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akizungumza kwenye maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei,
2016.
Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akisoma hotuba pamoja na ujumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Ban Ki-Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye
Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akiweka shada la maua kwenye mnara
wa mashujaa kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza
maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine yenye machafuko
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mkuu
wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Meja Jenerali, Elias Athanas akiweka shada la maua kwenye mnara wa
mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akiweka shada la maua kwenye mnara wa mashujaa kuwakumbuka
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha katika oparesheni
ya kulinda amani katika nchi zenye machafuko wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei,
2016.Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mkuu
wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Meja Jenerali, Elias Athanas akisalimiana na Mwakilishi Msaidizi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama mara
baada ya kuwasili katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016. Katikati ni Afisa Habari
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Picha
juu na chini ni Brass Band ikiongoza gwaride maalum la askari walinda
Amani kuingia viwanja wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.Manyama.
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Balozi wa nchi mbalimbali pamoja na viongozi wa Dini waliohudhuria
sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Katika
kutambua kujitolea kwa Tanzania kutoa askari wake kwenda kulinda amani
katika nchi zingine, Umoja wa Mataifa (UN) umesema unatambua huduma
inayotolewa na Tanzania ikiwa kama mwanachama wa UN na unafurahishwa na
hatua iliyopo ya kuendelea kusaidia kulinda amani katika operesheni
zinazofuatia.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama katika
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa
ambapo kwa nchini siku hiyo iliadhimishwa Dar es Salaam katika Uwanja wa
Mashujaa wa Mnazi Mmoja
Manyama alisema Tanzania imekuwa
ikijitolea kusaidia ulinzi wa amani katika mataifa mengine licha ya
kupoteza baadhi ya wanajeshi wake lakini bado wamekuwa wakiendelea
kujitolea kusaidia kuimarisha ulinzi wa mataifa mengine ambayo hali ya
usalama inakuwa siyo ya uhakika.
“Tumefurahishwa na historia ya
Tanzania ya kuzisaidia nchi jirani kulinda amani na kutatua migogoro ya
hapo zamani na kuziwezesha kujipatia uhuru,” alisema Manyama.
Aidha
Manyama alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kuendelea
kushirikiana na wanachama wake ili kwezesha upatikanaji wa amani kwa
mataifa yote na itaendelea kutoa heshima yake kwa wanawake na wanaume
ambao walipoteza maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine.
“Mwaka
jana idadi ya waliokufa ilikuwa 129, walinda amani hawa walitoka katika
nchi 50, wakiwa ni pamoja na wanajeshi, polisi, watumishi kutoka
mataifa mbalimbali, wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa na
watumishi wa ndani,
“Tunapenda kutoa heshima kwa mashujaa wetu
zaidi wanaume na wanawake milioni moja waliotumikia chini ya bendera ya
Umoja wa Mataifa kwa majivuno, weledi tangu kuanza kwa kazi hiyo 1948,”
alisema Manyama.
Nae mgeni rasmi katika siku hiyo, Meja Jenerali
James Mwakibolwa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa jinsi wanavyofanya
kazi na kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi na kuahidi Tanzania
itaendelea kutoa wanajeshi wake ili waendelee kulinda amani.
“Tumeshatoa
walinda amani 2,328 katika operesheni mbalimbali zilizopita na
tutandelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha amani na utulivu katika
maeneo mengine,” alisema Meja Jenerali Mwakibolwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni