Afisa
Usajili kutoka Rita Makao makuu Jijini Dar es salaam, Augustin Thomas
Mbuya ,ambaye ndiye mtaribu wa zowezi la Kampeni ya kitoa huduma
Rita,Akizungumza na wananchi Jijini Arusha ambapo kampeni hiyo
imezinguliwa rasmi.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu,ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa Kampeni ya Rita , ambapo imeanza rasmi katika Wilaya ya
Arusha Mjini na itaendelea kwa siku nne.
Muwakilishi wa Rita Mkoa wa Arusha Janeth Mandawa.
Afisa
Usajili kutoka Rita makao makuu Jijini Dar es salaam Joseph Mwakatobe
akizungumza na wananchi ,akitoa maelekezo namna ya kuandika wosia na
umuhimu wa kuhifadhi wosia.
Afisa Usajili kutoka Rita Makao Makuu Grace Shao.
Wananchi kutoka katika Wilaya ya Arusha Mjini wakfuatilia mafunzo
Na Mahmoud Ahmad Arusha
wananchi wametakiwa kuepuka dhana potofu kuwa kuandika wosia ni
Uchuro,jambo ambalo siyo kweli bali kuandika wosia ni kuepusha usumbufu
na migogoro kwa ndugu watakaokuwa wamebaki aidha watoto au mjane pindi mlegwa anapokuwa amekufa .
Hayo
yamesemwa na Afisa Usajili kutoka Rita Joseph Mwakatobe katika
ufunguzi wa zowezi la kampeni ya kutoa huduma za Rita kwa wananchi
,kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuandika wosia, namna ya kuhifadhi
wosia.
Joseph
amesema kuwa mara nyingi wosia ni muhimu sana kuandikwa kwasababu
inawarahisishia wale wanaobaki kuepusha kunyimwa haki zao ,kudhulumiwa
,Rita inawashauri wananchi kuandika wosia,kwani watu wengi hawana elimu
ya kutosha juu ya wosia.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amewahasa Rita wawaelimishe
wananchi sheria ya mirathi pamoja mwongozo,pia wawasaidie wananchi
kufahamu na kuelewa maeneo sahihi ya kuhifadhi wosia
Nkulu
amesisitiza kuwa mtu akiandika wosia ni vizuri zaidi maana ndiye
anayejua mali zake, na pia anamfahamu mtu sahihi wa kumpatia urithi
huo,na hii itaepusha migogoro na migongano ambayo ingeliweza kujitokeza.
Naye
Mratibu wa zowezi la kampeni hiyo Augustin Mboya amesema kuwa lengo kuu
la kampeni hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi waifahamu umuhimu
wa.kuandika wosia nakuhifadhi, watambue kuwa ile dhana ya kuwa kuandika
wosia ni Uchuro na kujitabiria kifo ni potofu na haina mashiko yeyote
,Pia watambue kuwa mtu anayeandika wosia lazima awe na akili timamu
,bila kusahau kuwa wosia huandikwa kwa hiari na siyo kulazimishwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni