Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa jukwaa la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber.
Baadhi ya waanzilishi na wadau usafiri wa Uber wakiwa katika uzinduzi usafiri wa uber  jijini Dar es Salaam leo.
JUKWAA la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber lazindua  usafiri wa Uber  jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la urahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits  amesema kuwa jukwaa
 la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo 
maarufu vya usafiri barani Afrika, mafanikio ya Uber katika nchi nyingi 
imeshazinduliwa na kuwa na mafanikio makubwa.
“Tunajivunia
 kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua. 
Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo 
huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa 
kuaminika.”Amesema Lits.
Lits amesema kuwa kwa kutumia usafiri huo 
wasafiri
 watasafiri kwa muda muafaka ukiwa na program ya maombi ya 
usafiri(Application), kwa kubonyeza tu kitufe ambacho kitatoa taarifa 
kwa dereva aliyepo karibu pia amesema kuwa Uber husaidia 
watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe pia hakuna kusubiri 
barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta 
basi. 
    
Amesema kuwa hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri 
usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo 
ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani
 kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu 
muda wa usiku.   
    
Safari hazina kificho mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina 
lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama 
kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva 
anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana
 na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna 
mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua. 
“Uber 
ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar 
es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye 
nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma
 yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar 
es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha 
abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”amesema.
ZIARA YA KIKUNDI CHA WAFANYA BIASHARA WANAWAKE TANZANIA, NCHINI COMORO TAREHE 14 JUNI 2016
Kikundi
 cha wajasirimali wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women 
Enterprenuers) kinachoongozwa na Bi. Anna Matinde Mkurugenzi wa Bodi ya 
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania waliwasili nchini Comoro kwa ajili ya 
ziara ya siku mbili. Lengo la ziara hiyo ni kutafuta masoko kwa ajili ya
 bidhaa za kutoka Tanzania, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa 
Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za 
biashara kati ya Tanzania na Komoro.
Wajasirimali
 hao waliwasili nchini Komoro tarehe 13 Juni 2016 na kupokelewa na 
 Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Wakati 
wakiwa nchini Komoro, wajumbe walipata fursa ya kukutana na wajumbe 
kutoka sekta binafsi ya Komoro pamoja na wa Tanzania waishio Komoro 
(Diaspora). Ujumbe huo ulifurahishwa sana na fursa za biashara zilizopo 
Komoro ambapo walielezea kuwa wapo tayari kushirikiana na Wakomoro 
katika kuleta bidhaa mbalimbali katika soko la Komoro.
Aidha,
 wajumbe walipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya 
Watanzania waishio Komoro (TADICO). Katika majadiliano yao, wajumbe 
waliweza kushaurina juu ya mikakati ya kufanya biashara nchini Komoro, 
ambapo Bi. Matinde aliwaaelezea wanadiaspora wasisahu pia kuekeza 
nyumbani kwani nako kuna fursa nyingi hivyo ni muhimu kwa wanadiaspora 
kuangalia namna gani na wao wanaweza kunufaika na fursa hizo.
Wajumbe
 pia walipata fursa ya kuonyesha na kutangaza biashara zao kwa 
wafanyabiashara wa Komoro ambapo walionyeshwa kuvutiwa sana na bidhaa za
 kutoka Tanzania. Ikumbukwe kwamba Komoro ni nchi ambayo hutegemea kwa 
kiasi kikubwa bidhaa zake kutoka nje. Biashara kati ya Tanzania na 
Komoro imekuwa ikikuwa siku hadi siku hata hivyo, bado kuna mahitaji 
makubwa ya bidhaa za chakula na imeonekana kuwa Tanzania ndio nchi iliyo
 katika nafasi nzuri kukidhi mahitaji hayo, kutokana na ukaribu wa nchi 
hizo kijiografia na kimila.
Sambamba
 na hilo, kikundi cha wajasirimali wanawake kutoka Tanzania wanatarajia 
kutiliana saini mkataba wa ushirikiano (Memorandum of Understanding) 
baina yao na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Komoro. Katika 
maelezo yake, Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Mhe. Chabaka Kilumanga 
alieleza kuwa huu ndio wakati muafaka wa vikundi hivyo vikaanza kufanya 
kazi kwa pamoja na kujuana ili kuweza kuboresha na kukuza wigo wa 
biashara kati ya Tanzania na Komoro. Alieleza pia kuwa ubalozi 
utaaendelea kushirikiana na wanadiaspora iwapo watapendelea kufanya kazi
 kwa pamoja na wajasirimali hao.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Chabaka Kilumanga akichangia mada katika warsha hiyo.
Bi. Anna Matinde, Mkurugenzi Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania.
Kikundi cha Wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania wakiendelea kusikiliza mada.
Mkuu wa Utawala na Fdha Ubalizi wa Tanzania Komoro Bw.Mudrick Soragha alievaa tai nyekundu akikaribisha wageni.
Wadua wakilendelea kuangalia bidhaa kutoka Tanzania, katika ofisi za ubalozi, Moroni.
wafanyakazi wa Ubalozi katia picha ya pamoja na kikundi cha wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania.
Wafanyakazi wa Ubalozi katika picha ya pamoja na wana Diaspora wa Komoro.
wajasiriamali wa Komoro wakiangalia bidhaa kutoka Tanzania.
Wajumbe kutoka Sekta Binafisi Komoro wakisikiliza kwa umakini mada.












Hakuna maoni:
Chapisha Maoni