Naibu 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline  
Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la 
Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika 
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.  
Naibu
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline  
Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa 
katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique).
 Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde
 Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James 
Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter 
Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia). 
Mkurugenzi
 Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara 
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili 
kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter 
Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali 
zilizowasilishwa. 
Mchoro
 huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa 
Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama 
Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika 
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza 
kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.  
Naibu
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline  
Mabula akiwa meza kuu baada ya Tanzania kuteuliwa na kuidhinishwa na 
Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja kuwa mwenyeji wa 
Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.Kulia kwa Naibu 
Waziri ni Waziri wa NIshati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde 
Raji Fashola ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Wajumbe
 kutoka nchi 44 za Afrika na wageni waalikwa kutoka nchi na mashirika 
mbalimbali ya Kimataifa wakiendelea na Mkutano wa 35 wa Shirika la 
Makazi la Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini 
Abuja, Nigeria. Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba 
na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula
Naibu
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline  
Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni katikati
 ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria mara 
baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika 
(Shelter Afrique). Kutokana na hali ya amani katika nchi hiyo, Naibu 
Waziri alipata ulinzi wa kutosha kama inavyoonekana alipopiga picha ya 
pamoja na walinzi walioandamana na wageni kutoka nchi mbalimbali katika 
ziara hiyo. Tudumishe amani yetu Tanzania.
Wajumbe
 wa Mkutano wa 35 wa Shelter Afrique wakiwa katika eneo la centenary 
city unaotarajiwa kuwa mji wa kibiashara Jijini Abuja mji ambao 
unajengwa na serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na sekta binafsi. 
Katika 
kutambua mchango wa Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na 
kuweka mbele utu wa binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, 
wajumbe kutoka nchi 44 za kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa 
Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua 
na kuiidhinisha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo 
utakaofanyika mwaka 2018.
Katika Mkutano Mkuu wa Abuja changamoto
 iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia wananchi wake 
nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa serikali zao 
kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu. Aidha, wajumbe wa
 Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi wa Afrika kuweza
 kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo unaotokana na vipato 
vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki nyumba za gharama 
nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya gharama nafuu, riba 
kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na ukosefu wa ardhi ya kujenga
 nyumba hizo.
Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika 
kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa 
katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo 
kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu umeazimia 
nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya nyumba kwa
 kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha 
bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano Saguya, 
Abuja, Nigeria). 
 
 
 
 
  
 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni