Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Jimbo
hilo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa
taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya
matibabu bure.
Wananchi
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati akizungumza katika
mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya
watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Tawi la Zanzibar, Ismail
Kangeta, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya matibabu itakayoanza kutolewa
bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa mkutano uliofanyika
Ofisi ya Jimbo.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mwananchi
wa Jimbo la Kikwajuni akisoma kipeperushi kilichotolewa na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya ambacho kina majina ya Hospitali ambazo wafaidika
wa huduma ya matibabu bure wanaweza kwenda kupata huduma hiyo wakati wa
mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo Kikwajuni Zanzibar.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza mmoja wa
wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero
mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo
hilo, Zanzibar.
Mwakilishi
wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Salim Jazeera (kulia), akimsikiliza
mwananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero
mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo
hilo, Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni