Gavana wa Jiji la Tokyo amesema
anajiuzulu baada ya kukabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha
za umma.
Gavana Yoichi Masuzoe amekuwa
akikosolewa mno kwa tuhuma za kutumia fedha za umma kwenda kutumbua
mapumzikoni, na kununua kazi za sanaa na vitabu vya watoto wake.
Gavana Masuzoe anatarajiwa kupoteza
katika kura ya kutokuwa na imani naye katika baraza la Jiji hilo kuu
la Japan baadaye hii leo.
Ziara za Gavana Masuzoe Jijini London na Paris pia zinadaiwa kutumia fedha za umma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni