Wabunge wa upinzani watoka wakiziba midomo na karatasi



Mbunge wa Vunjo kupitia NCCR Mageuzi James Mbatia akiwa anazungumza na waandishi wa habari Dodoma.
Wabunge wa upinzani katika muonekano .

Picha ikiwaonyesha Wabunge wa upinzani wakiwa wameziba mdomo ishara kuwa wamenyimwa kuongea na kuwasemea wananchi.


Dodoma. Wabunge wa Upinzani wameendelea kususia vikao
vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, huku leo
wakitoka bungeni kwa mtindo mpya wa kuziba midomo na
karatasi.

Hii ni wiki ya tatu mfululizo wabunge wa Ukawa wamekuwa
wakitoka bungeni baada ya kutangaza kuwa hawatahudhuria
vikao vyote vinavyoongozwa na Dk Tulia, kufuatia kukataa
hoja ya kujadili sakata la kufukuzwa wanafunzi 7,800 wa
stashahada maalumu ya sayansi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(Udom).

Wabunge hao wameeleza kuwa hawaridhishwi na uongozi wa
wa Naibu Spika na sasa wanaendelea na vikao vyao nje ya
Bunge.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi) James Mbatia amesema
wameanza kutoka kwa kufunga midomo na karatasi kuambia
dunia kuwa bajeti imejaa ghiriba na udanganyifu mwingi kwa
Watanzania.

Amesema watakwenda kuwaambia wananchi na hata kama
mikutano imezuiwa, Rais John Magufuli asitegemee kwamba
watanyamaza.

"Harakati hizi tulizianza tukiwa Chuo Kikuu na Dk Magufuli
nilikuwa naye japo alikuwa mbele yangu. Dk Ackson alikuwa
shule ya msingi na tangu wakati huo, harakati zinaendelea,"
amesema Mbatia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni