Timu ya taifa ya Iceland imepata
pointi muhimu katika mchezo wao wa kwanza katika michuano ya Euro
2016 dhidi ya Ureno katika kundi F, baada ya kutoka sare ya 1-1.
Katika mchezo huo Luis Nani
aliifungia Ureno goli na kuifanya iongoze lakini Iceland ilipambana
kiume na kusawazisha kupitia kwa Birkir Bjarnason.
Awali Cristiano Ronaldo alishuhudia
mpira wake aliopiga kwa kichwa ukiokolewa huku nao Iceland wakipoteza
goli dakika za mwisho baada mpira uliopigwa na Alfred Finnbogason
kuokolewa.
Birkir Bjarnason akisawazisha goli na kuiacha Ureno ikiwa na mshangao
Cristiano Ronaldo akiinamisha kichwa chini baada ya kuisha mchezo huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni