Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori
ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya Tembo
waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya
wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama
hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo
kutokana na ujangili basi watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo imeendelea kusema
kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa
kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo
zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40
iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa
ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa
kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha
hathari kubwa kiuchumi itakayotokea kutokana na kwamba Tanzania
kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka
ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika
pato la Taifa.
Pamoja na Hayo Serikali ya awamu
ya tano kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati
madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda
nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya
Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kushirikiana
na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa
ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa
la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka
Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni