Mwanaume mmoja nchini Japan
amebainisha kuwa hatimaye ameipata furaha yake kutoka kwa mpenzi wake
wa kike ambaye ni wa doli.
Mwanaume huyo Senji Nakajima, 61,
amedai kuwa anafurahi uhusiano wake huo usiona dosari na doli hilo
liitwalo Saori, ambapo wamekuwa wakifanya manunuzi pamoja na kutembea
naye.
Nakajima ambaye ameoa mwanamke na
amezaa naye watoto wawili, anaishi na doli hilo Jijini Tokyo, ambapo
amelisifia kuwa ni muaminifu na haumchuni fedha zake.
Senji Nakajima akiangalia TV na mpenzi wake doli
Senji Nakajima akimuogesha mpenzi wake huyo doli
Doli Saori likiwa limepozi mithili ya mwanamke mrembo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni