VIONGOZI WA DINI HUBIRINI AMANI KATIKA MATHEHEBU YENU :KAMANDA MKUMBO



 Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles  mkumbo akiwa anaongea na viongozi wa dini zote wa mkoa wa Arusha hii  ikiwa ni mkutano wa kwanza wa kufanya na viongozi wao tangu kuwasili mkoani hapa
 picha ya juu na chini ikionyesha baadhi ya mashehe ,askofu,wachungaji ,madiwani pamoja na maaskari waliothuria katika mkutano ulioandaliwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongea na viongozi wa dini juu ya namna gani ya kuendelea kudumisha amani ya nchi na mkoa kwa ujumla mkutano uliofanyika katika ukumbi wa polisi mesi uliopo jijini hapa

 Habari picha na Mahmoud Ahmad,Arusha

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles  mkumbo amewataka
viongozi wa dini mkoani Arusha kuakikisha wanaubiri amani katika
nyumba zao za ibada ili kuweza kuweka hali ya usalama na amani katika
mkoa wa Arusha.


Aliyasema hayo juzi katika   kongamano la siku moja la viongozi wa
dini mkoani Arusha katika kongamano la viongozi wa dini mkoa Arusha
lilondaliwa na kamanda mkumbo  na kuwashirikisha madiwani wa jiji la
Arusha pamoja na viongozi wa kisiasa .


Aidha kwa upande wake meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiwa kama
mmojawapo wa washiriki wa kongamano hilo na kueleza kuwa ujio
kongamano hilo liloandaliwa na kamanda Mkumbo ni kuonyesha mwelekeo
mzuri wa kulinda amani ya Arusha.

Aidha pia meya wa jiji la arusha alitumia muda huo kuwaasa
wafanyabiashara hususa ni wauzaji wa chakula pamoja na vinywaji vikali
kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa kufuata sheria ambapo alisema
kuwa airuhusiwi sehemu ambayo inauza chakula kuuza vinjwaji vikali
ikiwemo bia pamoja na pombe

"unaja sasa ivi tunataka tufanya mji wetu safa hairusiwi mtu anaeuza
pombe kuuza chakula na chakula kuuza pombe pia  kumekuwa na tatizo la
sehemu nyingi apa mjini kufungua mziki kama wanavyotaka sasa sasa hivi
airuhusiwi mtu yeyote kufungua mziki mkubwa iwe kwenye bar au grosary
pasipo kuwa na kibali rasmi kutoka sehemu husika hii pia inawahusu
hawa vijana ambao unakuta wanaingiza nyimbo kwenye cd yaani unakuta
kafungua mziki hadi kero  inakuwa usumbufu sasa kuanzia sasa hivi
airusiwi mtu kufungua mziki mkubwa pasipo kibali"alisema Kalist

Aidha alisema anaimani swala hili litafanikiwa kwakuwa polisi
wameshaamua  kushirikiana nao na watafanya kazi kwa umoja hadi
waakikishe mji wao unakuwa tulivu na msafiki .


Wakati huo huo mchungaji wa kanisa la Angilkana mchungaji  Kenoni
Kajembe alisema kuwa wao  kama  viongozi wa dini mkoani hapa wana
jukumu kubwa la kuakisha kwamba dhima ya amani inajulikana kwa waumini
wao wanaowaongoza.


Kongamano kama hilo linatarajiwa kufanyika mfululizo katika wilaya
sita zilizobakia za mkoa wa Arusha na wiki  hii na na pia  kamanda
Mkumbo anatarajiwa kufanya kongamano la amani kama hili na viongozi wa
serekali za mitaa ndani ya jiji la Arusha.


 mashehe kutoka katika misikiti mbalimbali ya mikoa wa Arusha wakiwa ktika picha ya pamoja na  kamanda wa polisi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha akiwemo meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
 wachungaji kutoka katika mazehebu mbalimbali wakiwa  katika picha ya pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha pamoja na meya wa jiji 

pia kamanda wa polisi mkoa wa Arusha aliwataka baadhi ya waandishi wa habari waliouthuria katika mkutano huo kupiga na viongozi hao picha ya pamoja hapa waliosimama nyuma wote ni waandishi wa habari waliouthuria siku hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni