Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.
Waziri
wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la
viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha
ifikapo July moja wanamaliza bidhaa zote bandia na zilizo chini ya
viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo
kuteketezwa.
Tamko
hilo amelitoa waziri Charles Mwijage lwakati alipokuwa anatembelea
kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake
katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya
Dangote ,Afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa
cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wakati
huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao
akiwemo Maofisa masoko afisa mkuu wa masoko wa AZANIA Naifa Abubakari
pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM wamemuhakikishia waziri wa viwanda
biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa
bidhaa zinazokidhi viwango bora na zenye ushindani na masoko kote
duniani
Aidha
kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na
vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan
amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL wataakikisha
wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni