Na.Catherine Sungura, WAMPUM-Monduli
Wilaya ya Monduli inatarajia kutoa kingatiba ya ugonjwa wa
trakoma(vikope) wa watu wapatao 140,962 kwa ngazi ya jamii kaya kwa
kaya hadi ifikapo mwezi julai mwaka Huu
Haya yamesemwa leo Na mkuu wa wilaya ya Monduli Fransic Miti
wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji dawa katika kijijo cha
Losingirani wilayani hapa
Miti alisema kila mtu yupo katika hatari ya kupata
maambukizi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele”napenda
kusisitiza kila mwanajamii ahakikishe kila mtu katika familia anatumia
dawa hizi ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi ambayo ni tayari
katika jamii yetu
Aidha aliahidi kulisimamia zoezi hili ipasavyo katika ngazi
zote kwani vifaa vyote vya utekelezaji wa zoezi hili vimeshawafikia
katika wilaya Nzima
Mkuu wa Wilaya alisema kwa mwaka uliopita wilaya yake
imetekeleza zoezi la ugawaji wa dawa za kudhibiti magonjwa ya kichocho
na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kwa ufanisi
mkubwa ambapo kati ya watoto 29,427,watoto 28,205 walipatiwa kingatiba
ambayo ni sawa na asilimia 95.8
Hata hivyo alisema kwa zoezi la mwezi wa tano mwaka huu la
umezaji dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto 31,150 sawa na asilimia
97.3 kati ya watoto 32,000.
Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa
Hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Upendo Mwingira alisema maambukizi ya
ugonjwa wa vikope(trakoma) upo kwa kiwango cha juu kwenye maeneo ya
wafugaji ambapo asilimia 57 ya watu waliofanyiwa utafiti mwaka 2004 hadi
2006 ilionesha wana tatizo la vikope hasa wilaya ya Monduli,Longido
pamoja na Ngorongoro.
inakadiliwa hadi kufikia mwaka 2020 dunia nzima iwe imetokomeza ugonjwa huu kwa kugawa dawa ambazo ni tiba na kinga
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni