Na Woinde Shizza,Arusha
CHUO
 cha ufundi Arusha, ATC, kinatarajiwa kukamilisha matengenezo ya 
Helkopita na kuirusha angani mapema mwaka 2018 na kuwa ni chuo cha 
kwanza nchini kurusha Helkopita iliyotengenezwa na Mhandisi mzawa.
Hayo
 yameelezwa jana na Mhandisi wa ufundi aliyebuni na  anayetengeneza 
Helkopita hiyo, Abdi Mjema, kwenye hafla ya chuo hicho kukabidhiwa 
maabara ya maji mwendo ambayo imejengwa na serikali ya Japan,kupitia 
shirika lake la misaada la JICA, chuoni hapo.
Mhandisi
 Mjema ,amemwambia katibu mkuu wa wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,
 Maimuna Tarishi, kuwa matengenezo ya Helkopita hiyo ambayo ameibuni 
yamefikia asilimia 40, na anafanya matengenezo hayo kwa kuwasiliana na 
mamlaka ya viwanja vya ndege kwa kila hatua anayofikia.
Amesema
 hatua ya majaribio ya kuirusha Helkopita hiyo ambayo inatengenezwa kwa 
malighafi za nchini anatarajia kuyafanya wiki tatu zijazo  mara baada ya
 kukamilisha hatua iliyopo sasa ambapo ni 40% ya matengenezo na ambapo 
utengenezaji wa Helkopita hiyo anatarajia kuukamilisha mwishoni mwa 
mwaka 2017 .
Mjema,
 ambae ni mtaalamu wa mitambo aliyebobea  pia mhadhiri wa chuo hicho cha
 serikali cha ufundi,amesema wazo hilo la kubuni Helkopita hiyo aliibua 
kutokana na changamoto za usafiri zilizopo nyumbani kwao wilayani 
Mwanga, ambayo eneo kubwa ni milima na wakati wa masika maeneo mengi 
huwa hayafikiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni