Na Mahmoud Ahmad,Arusha
BUNGE
la Jumuiye ya Afrika Mashariki limemwagiza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo
ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli
kuwachukulia hatua kali mawaziri wote wanaohusika katika wizara
zihususuzo Jumuiya hiyo kwa kutokuhudhuria vikao vya Bunge hilo.
Pamoja
na hilo pia imebainika kuwa kutokuhudhuria kwao kwenye vikao hivyo ndio
chanzo cha wananchi wa Jumuiya hiyo kutojua mambo mengi yahusuyo
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo
yamesemwa kwa masikitiko makubwa na mwenyekiti wa kamati ya sheria
katika Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mbunge kutoka nchini
Kenya,Peter Mathuki alipokuwa akielezea masikitiko yake kuhusiana na
mawaziri hao kushindwa kutikmiza wajibu wao.
Mathuki
ameeleza kuwa tatizo lililopo kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki la kutokuijua vema Jumuiya hiyo ni kutofahamishwa mambo mengi
yahusuyo Jumuiya na watu wenye wajibu huo ni mawaziri husika.
Ameongeza
kuwa kwa kipindi kirefu sasa mawaziri hao hawajatokea wala kushiriki
vikao vya Bunge hilo japo wanatakiwa kufanya hivyo ili kuweza kufikisha
ujumbe kwa wananchi ambao ndio walengwa wakubwa katika kujua mambo
mbalimbali ya nchi zao.
Mathuki
amedhamiria kuletamuswada katika Bunge hilo utakaoazimia kuwakataa na
kuwafukuza Bungeni hapo mawaziri wote hao ambao kwa mujibu wake anadai
wameonyesha utovu wa nidhamu kwenye Bunge hilo.
Katika
suala jingine, Mathuki amezungumzia umuhimu wa kutumia lugha ya
kiswahili katika vikao mbalimbali vya Bunge hilo ambapo pia imeonekana
ni sababu tosha kwa wananchi wengi kutojua mambo mengi ndani ya Jumuiya
kutokana na ugumu wa lugha ya kiingereza inayotumika na kongeza kuwa
inatakiwa kutumika sasa.
Amezitaka
nchi zote kwa kutambua na kukienzi kiswahili wanatakiwa kuhakikisha
kinakuwa ni lugha ya kila Taifa na itumike katika kufundishia mashuleni
na hata katika matumizi ya kila siku ya lugha hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni