Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akitia saini kitabu cha Wageni alipotembelea Kata ya Mbweni
iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli za upandaji mikoko
katika eneo hilo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi
katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni
katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni
kesho
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya mazingira hapo tarehe 5 juni.
.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.
January Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni
ambao walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni
jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya
kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya
Mbweni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa Wananchi wa
Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira.
Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika katika
fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza
Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba
alisititiza pia Wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda
mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.
Wakisoma Risala yao , Wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi kwa
ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia
changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo
mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.
Mwisho
Waziri aliwahukuru Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye
katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni
kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5
juni kila mwaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni