Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya
Magazeti ya Serikali (TSN)
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa
Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel
Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni