Mkali wa masumbwi duniani, Mohammed Ali akimuangalia George
Foreman akiwa chini baada ya kumpiga sumbwi lililomwangusha katika
raundi ya nane katika pambano lililofanyika mwaka 1974 Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo zamani ikiitwa Zaire.
Bondia Mohammed Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Ali
ambaye alhamisi alikimbizwa hospitali kwa matibabu, alikuwa na matatizo
ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson,
ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemeka kila mara.
Alifariki katika jiji la Phoenix Arizona
Mohammad Ali akimpongeza mtoto wake Laila baada ya kushinda pambano lake la masumbwi. Laila alifuata nyayo za baba yake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni