TAREHE
14.06.2016 MAJIRA YA SAA 10:30HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE KATA YA BUGOGWA
WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO
WALIFANIKIWA KUMKAMATA JONATHAN GABRIEL MIAKA [31] MKAZI WA BUGOGWA
AKIWA NA MISOKOTO MIA NNE [400] YA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA
SHERIA ZA NCHI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAFANYA
BIASHARA YA KUUZA MADAWA HAYO YA KULEVYA KATIKA MITAA MBALIMBALI YA
IGOMBE NA ILEMELA PIA, NA PINDI MTUHUMIWA ANAKAMATWA ALIKUWA AKIFANYA
MAWASILIANO NA WATEJA WAKE JINSI YA KUWAPATIA BHANGI HIYO.
KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE
TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA SAA 13:30HRS KATIKA ENEO LA MWANANCHI WILAYANI
NYAMAGANA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA RAMADHANI HAMAD
MIAKA [24] MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA BHANGI KILO TATU [03] KITENDO
AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA
AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA BIASHARA YA KUUZA BHANGI KATIKA MITAA
HIYO WANAYOISHI, NDIPO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA POLISI NA KUFANIKIWA
KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KILO HIZO ZA BHANGI.
WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI
YA ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU
WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA BHANGI UKIENDELEA, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU
MASHITAKA YANAYO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA
YA KULEVYA AMBAYO NI HARAMU NA BATILI KATIKA USTAWI WA NCHI YETU, KWANI
JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATAFUTA WALE WOTE
WANAOJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO NA KUWAKAMATA KISHA KUWAFIKISHA
KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA AJILI YA KUPEWA ADHABU KALI ILI IWE
FUNDISHO KWA WATU WENGINE.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni