Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akimuonesha Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye baadhi ya wachezaji
wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys
waliopatiakana kupitia michuano ya Airtel Rising Stars wakati wa
uzinduzi wa awamu ya sita ya michuano hiyo uliofanyika Dar es Salaam
Jumapili Juni 26 2016.
Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipinga mpira
kuashiria uzinduzi wa rasmi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016.
Uzinduzi huo umefanyika Jumapili 26 Juni 2016 kwenye makao makuu ya
Airtel Tanzania Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo
wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016 jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa katika picha
ya pamoja na viongezi wa TFF pamoja na Airtel Mara baada ya uzinduzi wa
Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars
Wafanyakazi
wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari,
Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu
wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars.
Airtel yazindua msimu wa 6 wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016
Dar es
Salaam, Jumapili 26 Juni 2016 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua msimu wa sita wa mashindano
ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars na
kuwapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Serikali pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini
(TFF) za kukuza mchezo wa soka.
“Programu
za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale
duniani. Ndiyo maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising
Stars ambayo matunda yake yameonekana dhahiri katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita”, alisema Nnauye.
Alitoa
mfano wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti
Boys ambayo wachezaji wake 10 wa kutumainiwa wametokana na Airtel Rising
Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars vilevile yanaoneka dhahiri
kwenye timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo wachezaji wake wote
wanatokana na programu hii ya vijana”, alisema Nnauye. Klabu za daraja
la kwanza na ligi kuu Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya Airtel
Risings Stars.
Waziri
amewataka viongozi wa soka kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel Rising
Stars ili kuweza kubaini vipaji vingi zaidi kupitia mashindano haya ya
vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu za wasichana na wavulana
kuanzia ngazi ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya Taifa jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa kampuni ya Airtel
Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo
imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo
huo marufu hapa nchini.
Alisema
Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya
Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana
kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel
Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana
kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano
cha kipato cha kuaminika”, alisema.
“Kwa
kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar, Airtel
Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia
mchezo wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa
Tanzania. Ni njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga
mkono”, alisema.
Kwa
upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya Airtel Rising
Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa soka
hapa nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono.
Naamini kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.
Airtel
Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa
itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke,
Arusha, Lindi na Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni