Katika
kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la
madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi
Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni
70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata
milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia
kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.
Akizungumza
katika halfa ya kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni
hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na
kusaidia kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia
taifa.
Hata
hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini kama watu matajiri nchini
wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati
nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na
sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa kusuasua.
"Ukisaidia
mtu mmoja katika elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama
watu matajiri wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza
tatizo hili linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.
Mkurugenzi
Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika
halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo
zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata
madawti 500.
"Matajiri
wanatakiwa kutambua kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu,
taifa na wananchi na hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo
wanaowasaidia kufanya biashara zao kwa amani," alisema Dk. Mengi.
Aidha
amewataka wakuu wa wilaya hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama
watakuwa hawajakamilisha na wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza
juhudi huku akiwashauri kuandaa mikutano katika wilaya zao na
kushirikisha wananchi wao ili waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo
kumalizika.
Kwa
upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa
wilaya ya Handeni, Husna Rajab wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao
amewapatia na kuwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama
jinsi amevyofanya Dk. Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.
Awali
kabla ya msaada ambao umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa
ikikabiliwa na upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na
tatizo la upungufu wa madawati 4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya
kupokea pesa kwa ajili ya madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake
kusaidia kupunguza tatizo la madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa
hundi ya milioni 35, Mkuu wa wilaya ya Haneni, Husna Rajab. Wa pili
kushoto ni Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa
Mji wa Handeni, Twaha Mgaya na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni,
Ramadhani Diliwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa
hundi ya milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya
ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi
Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Chalinze, Said Zikatimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni