Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa Tisa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za
Watu Wenye Ulemavu ( CRDP), umeanza jana
( Jumanne) hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, New York, Marekani.
Mada au ujumbe wa
Mkutano huu wa siku tatu ni “
Utekelezaji wa Agenda ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030) Kwa Watu
Wote Wenye Ulemavu: Pasipo Kumwacha Yeyote”
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu, unaongozwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dr.
Abdallah Possi ( Mb). Wajumbe wengine ni Mhe. Riziki Lulinda ( MB), Mhe. Elly
Macha ( Mb) ,Mhe. Stella Ikupa ( Mb) , Bi Josephine Lyengi, Kaimu Kamishna
kuhusu watu wenye ulemavu na Bi. Ngusekela Nyerere , Afisa Mambo ya Nje, Wizara ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Akizugumza wakati wa
majadiliano ya jumla mara baada ya hafla ya ufunguzi , Naibu Waziri. Dr.
Abdallah Possi amesema, changamoto kubwa inayowakabilia watu wenye
ulemavu nchini Tanzania, ni fursa za kiuchumi.
“Licha
ya
mafanikio kadhaa yakiwamo ya
utungaji wa sera, sheria na mabadiliko mbalimbali kuhusu watu wenye
ulemavu, bado kuna changamoto
nyingi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi
kwa lengo la kuwapunguzia matatizo watu wenye ulemavu yakiwamo matatizo
ya kutokuwa na fursa sawa na kuondokana na umaskini”. Akaeleza
Naibu Waziri
Na Kuongeza kwamba, Tanzania kama ilivyo kwa nchi yingine inakabiliwa pia na vipaumbele
vinavyokinzana na ambavyo ni muhimu
lakini vikiwathiri zaidi watu wenye ulemavu.
Akavitaja baadhi ya
vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja
na upatikanaji wa maji safi na salama, chakula, huduma za afya, elimu na ukosefu wa
ajiria.
Vile vile Naibu Waziri ameleza kuwa mtazamo
hasi kuhusu watu watu wenye ulemavu
ni changamoto nyingine ambayo inatatiza ujumuishi wa watu wenye ulemavu katika
fursa mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambazo wangeweza kunufaika nazo bila ya kujali hali zao.
Akizungumzia
kuhusu
mahitaji ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania,
Mhe. Dr. Possi, ameeleza washiriki wa mkutano huu kutoka nchi 164 ambazo
zimeridhia mkataba wa watu wenye ulemavu kwamba, watu wenye ulemavu
nchini Tanzania wanakabiliwa na tatizo kubwa la kutokuwa vifaa
saidizi ambavyo vingewasaidia na
kuwawezesha katika
shughuli zao za kila siku.
Vivile akabainisha
kuwa mwaka 2015, Tanzania ilikuwa
moja ya wadhamini wakuu wa Azimio kuhusu
watu wenye ualibino, azimio ambalo pamoja
na mambo mengine limelenga katika kutafutia ufumbuzi baadhi ya
changamoto zimazowakabili watu wenye
ualibino katika maeneo mbalimbali
yakiwamo ya elimu, afya na ajira.
“ Bila ya kuwa na
vifaa saidizi watu wenye ulemavu wa aina yoyote ile wanashindwa kupata fursa anuai ambazo kwayo
zingewawezesha kuishi pasi utegemezi na hivyo kuchangia katika yao
binafsi na maendeleo ya nchi yao”
akasisitiza Naibu Waziri. Na akatumia fursa hiyo ya kuhimiza upatikanaji wa vifaa saidizi kwa
watu wenye ulemavu ili wawe kujitegemea.
Awali
akifungua
mkutano wa tisa wa Mkataba wa Watu Wenye ulemavu, Rais wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft, amesema nchi
ambazo zimeridhia mkataba huo zinaowajibu wa kuchukua hatua zote
muhimu zikiwamo za
maendeleo jumuishi kwa watu wenye
ulemavu.
“ Kila nchi mwanachama
wa mkataba huu na asiye wamanachama anakazi ya kufanya, lakini katika
dunia ya leo mafanikio hayamo katika
mikono ya serikali peke yake” akasisitiza Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa.
Na kwa sababu hiyo, ametoa wito kwa serikali zote pamoja na
wadau mbalimbali kufanya kazi kwa
pamoja kwa lengo la kuwawezesha watu wenye ulemavu zaidi
ya bilioni moja.
Pamoja
na hotuba kutoka kwa
nchi wanachama, mkutano huu ambao ni wa siku tatu utakuwa na mijadala
ya pembezoni yenye mada tofauti. Mkutano huo pia unashirikisha Asasi
zisizo za kiserikali zinazojihusisha na masuala ya watu wenye
ulemavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni