fastjet,
 shirika la ndege la bei nafuu Afrika  limezifanya ndoto za 
usafiri  kuwa za kweli  kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili  waliopaa
 anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.
 Ukiwa
 kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi  kusafiri, 
fastjet  imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi  kuanzia 
Jumanne Mei 31 ataingia kwenye  bahati na nasibu  ya kwanza ya aina 
yake  ijumulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri 
bure   katika njia yoyote  ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.
Kwa
 watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo  shirika linawapa uwezo wa 
kwenda katika mapumziko  au kwenda katika safari ya manunuzi  pamoja na 
marafiki  na familia  jambo wamekuwa wakiliwazia  kila mara.
Ama
 kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza 
mahitaji ya biashara kwa kuokoa  gharama za usafiri katika safari 
nyingine kumi wanazozihitaji  kusafiri.
 “Ni
 rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi 
kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki  na 
familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa 
fastjet Tanzania John Corse.
 Njia
 ambazo zinahusiana  kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam 
kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka, 
Harare na Johannesburg hali kadhalika safari  kati ya Kilimanjaro na 
Harare.
 Tiketi
 zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na  za 
ndani  zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10.
 Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure  ni lazima 
zifanyike  kabla ya Desemba 11, 2016.
 Ikitambuliwa
 kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa 
inafanya safari  ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia
 ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri 
wa anga.
 “Usafiri
 wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa 
Tanzania  kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara  na 
watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse  na kuongeza, “tumezindua 
punguzo hili la nauli  hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea 
usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au 
mapumziko.”
Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au  malipo kwa njia ya mitandao ya simu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni