Basi la TAHMEED lililokuwa
likitoka mkoani Tanga kuelekea jijini Dar es salaam limeungua moto na
kuteketea kabisa maeneo ya Kabuku mkoani humo Habari zinasema abiria
wote wamenusurika katika tukio hilo baya lakini mizigo na basi lenyewe
vimeungua na kuteketea kabisa kwa moto kwa jinsi inavyoonekana katika
tukio hilo katika picha inaonekana moto ulianzia mwenye magurudumu ya
nyuma upande wa kulia kama inavyoonekana.
(PICHA KWA HISANI YA MITANDAO YA KIJAMII)
Hapa likionekana limeteketea kabisa na haikuwezekana kuzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni