Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa
pole Hussein Mkola ambaye ni mtoto wa marehemu Mkola Hussein ambaye
alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii
katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni
alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni
njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia
nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati
alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya
Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu
wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa
Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na
baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika
kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole
wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu
wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha
Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika
msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji
hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika
kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Davis Mwamunyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu kushoto), nyumba ya kwanza
katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa kuwa
majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa
pole katika familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika
Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa salamu
za pole kwa ndugu wa marehemu Mkola Hussein pamoja na wananchi wa
Kitongoji cha Kibatini kulipotokea mauaji kwa watu wanane ambao
walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii
katika Kitongoji hicho kilichopo Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Katika
hotuba yake Masauni alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo na
itahakikisha inawakamata wauaji wote waliofanya ukatili huo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
wakijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange kabla ya kwenda kutoa pole kwa familia ya wafiwa katika
Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga ambapo watu wanane
walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni