JUNE 5 SIKU YA MAZINGIRA KWA MKOA WA ARUSHA KWA KUPANDA MITI KWENYE MAENEO YA KIJAMII

Image result for rc arushaMahmoud Ahmad Arusha 
 MKOA wa Arusha, utaadhimisha siku ya mazingira duniani June 5 kwa kupanda miti aina mbalimbali ya matunda ,vivuli na ya asili kwenye shule za msingi na vyanzo vya maji ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
 
Katibu tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
 
Amesema shirika la umoja wa mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na kusimamia mazingira yao.
 
Kwitega,alisema mwaka huu 2016 maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa na kauli mbiu isemayo uvumilivu  ufike mwisho juu ya biashara haramu ya wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
 
Alisema kwa kuanza mkoa utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha, ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili  ambayo ni rafiki wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
 
Alisema maadhimisho hay mwaka huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la kuadimisha maadhimisho hayo ambayo kli mbiu yake  ya taifa inasema tuhifadhi vyanzo  vya maji  kwa uhai wa taifa  letu .
 
Kwitega, alisema  katika maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
 
Alisema siku ya kilele ya maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .
Jun 1 at 2:32 PM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni