Ellen Johnson Sirleaf kukabidhiwa tuzo ya Mo Ibrahim

Tuzo ya uongozi bora ya Mo Ibrahim kwa viongozi wastaafu barani Afrika kwa mwaka huu inakwenda kwa rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnston Sirleaf. Hafla ya kumtunuku inafanyika mjini Kigali Rwanda.
Mo Ibrahim ambaye amekuwa akitoa tuzo ya uongozi bora kwa viongozi wastaafu barani Afrika amesema bara hilo linakabiliwa na uongozi usiozingatia maslahi ya raia walio wengi huku sekta binafsi ikitelekezwa.
Tuzo ya uongozi bora ya barai Afrika ya Mo Ibrahim ya mwaka huu inatazamiwa badaye jioni ya leo kupewa Rais wa zamani wa Liberia Johnson Sirleaf. Hafla itaongozwa na  Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika, huku akiwepo Rais wa Ivory Coast Alassane Ouatarra ambaye ni mwenyekiti jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika yuko mjini Kigali kuhudhuria khafla hiyo.
Festus Mogae (picture-alliance/ dpa) Rais wa Botswana Festus Mogae, aliwahi kushinda tuzo ya Mo Ibrahim
Mo Ibrahim amesema kwamba kukosekana kwa utashi wa kisiasa na ukosefu wa uongozi kwa maslahi ya raia walio wengi ni jambo ambalo limezuia bara hilo kupiga hatua ya maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
"Hilo ni suala ambalo kamwe huwa halijadili wazi,nani anatoa huduma?nani anatoa elimu,nani anatoa ushirikiano kwenye kila sekta?Ni mwananchi ambaye serikali ambayo wakati haimzingatii kwenye sera zake,hao ni mashujaa ambao daima hatuwazungumzii, na wakati umefika tuwazungumzie", amesema Mo.
Tuzo ya Mo Ibrahim ya dola milioni tano za Marekani hupewa viongozi waliojitahidi kuweka mazingira ya uongozi bora ya utawala wakati wakiwa madarakani.
Hata hivyo tangu ilipoanza kutolewa tuzo hii mwaka 2007  alipotunukiwa  Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano wadadisi wanahisi haijaleta mabadiliko makuwa kwenye sekta za utawala bora barani Afrika, lakini Denittah Ghat ambaye kwenye bunge la Kenya anasema wakati kama huu ni nafasi nyingine ya viongozi kujitathmini ikiwa wanafanya vema katika uongozi.
Kenia Mo Ibrahim verkündet den Gewinner des Preises 2015 (picture-alliance/AP Photo/B. Curtis) Mo Ibrahim mwanzilishi na mwenyekiti wa wakfu wa Mo Ibrahim
"Hii ni nafasi nzuri nay a kipee na ninafurahi kwamba sasa tunakutana hapa kujadili hata nafasi ya mwanamke ktk uongozi barani Afrika tunafahamu kumekuwepo na udhaifu kwa baadhi ya serikali kuwapa nafasi wanawake ambao kimsingi ni wachangiaji wa zuri kwenye maendeleo lakini nadhani kukutana hapa nadhani ni fursa nyingine kulitathmini hili".
Kutolewa kwa tuzo hiyo kumefungua kikao cha siku tatu cha viongozi wa serikali na wale wa kiraia zaidi ya elfu moja kutoka barai Afrika wakijadiliana ushirikiano unaopaswa kuwepo baina ya serikali na sekta binafsi. Rais mstaafu  Sirleaf anapewa tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake katika  kurejesha amani na usalama nchini Liberia na pia hatua yake ya kutojiingiza kwenye siasa za ushawishi kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopita nchini Liberia ambapo mwanasoka wa zamani George Weah  alimshinda aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Joseph Boakai.
Ni tuzo ambayo hutolewa kwa viongozi walioondoka madarakani kwa mujibu wa katiba  au kwa utashi wao. Hata hivyo mwaka  2009,2010,2012,2013.2015 na 2016 jopo la majaji wa wakfu wa Mo Ibrahim lilishindwa kumpata kiongozi  aliyefaa kupokea tuzo hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni