NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
WANAWAKE
visiwani Zanzibar wameshauriwa kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa
lengo la kujiongezea kipato na kujiajiri wenyewe.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT)
Pily Khamis Lapda, amesema wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya
shughuli za ujasiriamali kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa
kufikia malengo yao ya kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.
Amesema
zipo njia mbali mbali za kuwakomboa wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda
na kuamini shughuli za ujasiriamali kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.Amewashauri
wanawake nchini kujiamini pindi wanapoanzisha biashara zao sambamba na
kujiwekea malengo ya kudumu ya kibiashara yatakayowasaidia kumiliki
mitaji mikubwa ya kibiashara.
Mkurugenzi
huyo Pily, akizungumzia malengo ya taasisi yake inayoendesha na
kusimamia mafunzo ya kuyajengea uwezo wa kitaaluma makundi mbali mbali
ya kijamii ili kupata uwezo wa kutumia ipasavyo fursa za ujasiriamali
wenye maendeleo.“Wanawake
tuwe mstari wa mbele kujifunza mbinu mbali mbali za kujikwamua
kiuchumi, pia tujitume na kuwa wabunifu katika biashara zetu ili nasi
tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.
Akitoa
mada ya Uvumbuzi binafsi, mtaalamu wa Saikolojia na maendeleo ya
vijana, Joseph Mrindo amesema wanawake waliopo katika sekta ya
ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya ujasiriamali mdogo mdogo
kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na kushindwa kufikia
malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.
Ameeleza
kuwa Zanzibar ni sehemu muhimu yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake
wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kujiongeza kibiashara.Mtaalamu
huyo, amewasihi wajasiriamali kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za
maendeleo ya kibiashara ili wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha
kupewa mikopo kwa wakati na benki mbali mbali nchini.
Naye
mshiriki wa mafunzo hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wajasiria mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi
wa kufanya biashara zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.Mafunzo
hayo ya siku mbili yanatolewa na taasisi ya New vision consortium
(NVCT)iliyopo Zanzibar na jumla ya washiriki 200 kutoka taasisi binafsi
na za umma wanapewa ujuzi huo wa ujasiriamali.
Wadhamini wa mafunzo hayo ni pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na IQUITY BANK
MKURUGENZI
wa New vision consortium Pily Khamis Lapda(aliyekaa katikati) akifungua
mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar
yaliyofanyika katika Skuli ya Haile-Sela-ssie.
BAADHI
ya washiriki katika mafunzo hayo kutoka taasisi binafsi na za umma
wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo
hayo, huko Skuli ya Haile-Sela-ssie.
MSHIRIKI
wa mafunzo ambaye pia ni mjasiria mali kutoka U.WT. jimbo la Mwera
Salama Mohamed Tahir akichangia mada ya uvumbuzi binafsi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni