Na Jumbe Ismailly, IKUNGI
IDADI
ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilaya ya
Ikungi waliokosa makazi kutokana na nyumba zao kuanguka kufuatia mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa zimeongezeka kutoka kaya 22
zanye zaidi ya wakazi 154 hadi kufikia kaya 177 zenye zaidi ya wakazi
700 baada ya nyumba189 kuanguka.
Ongezeko
la idadi hiyo ya wakazi linatokana na mvua kubwa iliyonyesha apr,16
hadi 18,mwaka huu na kusababisha mto kuacha njia yake na kulenga katika
Kitongoji cha Mwasusu,na ndipo kaya 22 zenye zaidi ya wakazi 154 katika
vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,Kata ya Mwaru kukosa makazi baada ya
nyumba 34 kuanguka.u
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Mwaru,Hamisi Malongo alisema hayo alipokuwa akitoa
taarifa za athari zilizotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi
sasa Mkoani Singida na kuongeza kwamba pamoja na nyumba hizo vile vile
makanisa matatu ya FPCT na AIC yalianguka kufuatia mvua hizo.
“Na
tuliloligundua sisi kama viongozi kama serikali upande wa kata kwamba
vijiji vya Kaugeri na Mduguyu ni vijiji vya mpakani na Mkoa wa Tabora
ambavyo ndiyo bonde la Mto Wembere unapita kwa hiyo mvua inaponyesha
pande zote za dunia kwa hiyo wao ni rahisi sana kuathirika na mvua
hizo.”alisisitiza Malongo.
Naye
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugeri,Laurence Bomba Torokoko
akizungumzia hasara zilizotokana na mvua hizo alizitaja kuwa ni pamoja
na nyumba 105 zenye wakazi 412 walikosa makazi kabisa ya kuishi na
hekari 92 za mazao mbali mbali.
Madhara
mengine kwa mujibu wa Torokoko magunia 334 ya mpunga na mtama,kuku 20
na ng’ombe moja amba hatha hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali
kuwasaidia familia zilizoathirika kutokana na mvua hizo ambazo bado
zinaendelea kunyesha.
Kwa
upande wao baadhi ya waathirika wa mvua hizo,Mchungaji,Hosea Eliudi
licha ya kuishukuru serikali kwa msaada wa awali lakini hakusita kueleza
changamoto zinazowakabili kwenye kambi hiyo kuwa ni hatari ya kuugua
ugonjwa wa malaria kutokana na kuwepo kwa mbu wengi huku wakiwa hawana
vyandarua baada ya walivyokuwa wakitumia kuangukiwa na nyumba zao.
Misaada
pamoja na changamoto zingine kwa mujibu wa mchungaji huyo ni mahema
makubwa yatakayoimarisha kambi hiyo kufanana na zile za wakimbizi na
kuzitaja changamoto zingine kuwa ni kushindwa kuvuna kwa kuwa hawana
sehemu ya kuhifadhi mazao yao.
Mashiri
Masunga mkazi wa ni mmoja waathirika wa mafuriko ya mvua hizo kwa
upande wake anaelekeza shutuma zake kwa Mbunge wa jimbo la Singida
Magharibi,Elibariki Kingu kwamba licha ya kuwaahidi kuwapelekea kadi za
CCM pamoja na maturubai tangu apr,23,mwaka huu lakini wamejikuta
wakiende na matatizo ya kutokuwa na kifaa hicho muhimu kwa kujikinga na
mvua.
Mmoja
wa wananchi walioathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha akiwa
kwenye makazi yake mapya yaliyopo kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha
Kaugeri akihofia wingu lililotanda kama alivyokutwa na kamera ya kituo
hiki(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi
ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilayani
Ikungi wakihamisha baadhdi ya vitu vilivyosalia kwenye makazi yao ya
zamani na kuhamia kwenye eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya
wahanga hao wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa sisku tatu
mfululizo na hivyo kusababisha zaidi ya wakazi 700 kukosa mahali pa
kuishi
Ni
Miundombinu ya barabara ya kutoka Mlandala kwenda kwenye Kitongoji cha
Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wahanga wa
mafurriko ya mvua zilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha Mkoani Singida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni