Muigizaji wa Bongo movie Salma Jabu 'Nisha' anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.
Siku ya Alhamis msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha alikuwa anamtongoza Young Dee.
Amber Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku akikiri kuwa Nisha ni fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.
Baada ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:
"Mimi sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka kuingia kwenye muziki hivyo Young Dee kama msanii wa Bongo fleva alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.
" Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni