Kamati
ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, inatarajia kuwahoji mwanahabari
Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la kila wiki, la Raia Mwema kwa
madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge, Aprili 9 wiki hii.
Hayo
yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai
aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi
ya bunge.
Hayo
yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba
mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na
gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?”
haidhalilishi bunge.
Spika Ndugai leo Aprili 12, ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni