Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba
(kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu
Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko
kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi
katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani
tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala
ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama
na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28
Aprili kila mwaka.
Maadhimisho
haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA)
nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na
maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni
leo tarehe 29.
Mgeni
Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani
Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa
ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja
ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na
kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi.
Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani
Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala
ya afya ya usalama mahala pa kazi.
Aidha,
akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko
kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja
na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona
ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho
kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa
kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote
ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili,
kulipia michango na kufuatilia michango yao.
Mfuko
umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi
katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika
tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018.
Katikati
Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya
kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya
Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe
pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw.
Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja
aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja
vya Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi
wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto),
Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo
huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo,
Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina
Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi
wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa
ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa
Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa
Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili
na cha ushiriki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni